loader
Dstv Habarileo  Mobile
China: Hatudhamirii kuitawala Afrika

China: Hatudhamirii kuitawala Afrika

CHINA imesema, haina lengo la kuzitawala nchi za Afrika kupitia misaada ambayo imekua ikiitoa, ila kuzisaidia nchi zinazoendelea kuinua pato la taifa kumaliza umasikini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Beijing.

Amesema kwa muda mrefu, China imekua na ushirikiano mzuri na nchi za Afrika hasa katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo miundombinu, huduma za kijamii, biashara, masuala ya kidiplomasia, na kwamba wanatarajia mahusiano hayo yataendelea kwa manufaa ya pande zote.

Wang ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo tetesi katika mitandao ya kijamii na kuripotiwa na vyombo vya habari barani Afrika kwamba misaada mingi ambayo taifa hilo la pili kwa uchumi duniani limekua likiitoa, ina lengo la kuzidhoofisha nchi zinazoendelea.

“Nchi za Afrika ni marafiki wetu wakubwa ambao tumekuwa tukishirikiana nao kwa kipindi kirefu, sio kweli kwamba China inataka kutawala Afrika, lengo kubwa ni kuleta ushirikiano wenye tija kwa manufaa ya Afrika na nchi ya china,” amesema Wang.

Katika mkutano huo Wang, alitumia muda mwingi kupokea na kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari na akasema kuwa, ni muhimu kwa mataifa yote kuendelea kushirikiana kuleta maendeleo ya kweli.

“Tunahitaji maendeleo ya kweli na hayo yatafikiwa endapo tu sote tutajizatiti na kufanyia kazi malengo tuliyojiwekea ikiwemo uekelezaji wa miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ambao utaleta mapinduzi katika sekta ya biashara na usafirishaji”amesema.

Mwanadiplomasia huyo amesema, moja ya mipango ya mwaka huu ni kuhakikisha maazimio yote manane yaliyofikiwa mwaka jana katika mkutano wa jukwaa la ushirikiano kati ya Afrika na China yanafikiwa.

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika umekuwa na tija kubwa na ameunga mkono kauli ya Waziri Wang kuwa misaada ya China kwa nchi zinazoendea haina nia hasi.

“Hizo zote ni propaganda zinazoenezwa na mataifa yasiyozitakia mema nchi za Afrika, hawataki Afrika iendelee,”amesema Balozi Kairuki.

“Ukiangalia kwa undani utaona kwamba nchi zinazoeneza propaganda hizo ndio zenyewe ziko mstari wa mbele kufanya biashara na China, hii inashangaza”amesema.

Waziri Wang amesema China itaendelea kuziunga mkono kampuni za ndani ambazo zinazokumbwa na misukosuko na akatoa mfano wa kampuni ya simu ya Huawei ambayo imeshitakiwa na Marekani.

“Kwa vyovyote vile lazima tuwe upande wa kampuni yetu ya Huawei, tunajua ni kampuni nzuri ambayo inafanya kazi kubwa katika kukuza teknolojia,” amesema na kuongeza kwamba wanaamini kesi hiyo itaisha salama.

Huawei ambayo ni moja ya kampuni kubwa za mawasiliano na usambazaji wa simu duniani, hivi karibuni ilifunguliwa mashitaka na serikali ya Marekani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha, kuzuia utekelezaji wa haki, na wizi wa teknolojia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/aef05caab1f9c38f3362c88a5cfcff6e.jpg

MZOZO umeibuka nchini Somalia juu ...

foto
Mwandishi: Deogratius Kamagi, Beijing

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi