loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Punda tu kubeba abiria, wagonjwa

MAMLAKA ya mji mkuu na mkongwe wa kisiwa cha Lamu uliopo pwani ya Kenya wenye wakazi takribani 10,000, umeendelea kupiga marufuku ya matumizi ya vyombo vya usafi ri vya moto yakiwemo magari na pikipiki.

Magari pekee yanayoruhusiwa katika kisiwa hicho cha kihistoria, kinachovutia watalii kila kukicha ni ya mkuu wa wilaya, gari la Polisi, gari la kubeba wagonjwa na gari la mamlaka ya maji. Pia trekta la kuzoa taka linaruhusiwa.

Kwa wengine, usafiri pekee unaoruhusiwa ni matumizi ya punda na mikokoteni. Asilimia kubwa hutembea kwa miguu, miaka nenda miaka rudi.

Punda, mbali ya kubeba watu kwa maana ya abiria au wamiliki wake, wakati mwingine hubeba pia wagonjwa, magunia yenye bidhaa mbalimbali na hata vifaa vya ujenzi.

Na kutokana na umuhimu wake, wamekuwa ghali. Hutunzwa vyema, huku wamiliki wa wanyama hao wakifananishwa na watu wanaomiliki magari madogo ya kutembelea au yale ya kubeba mizigo.

Kwa mujibu wa Gavana wa Lamu, Dk Issa Timamy, ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza chombo cha usafiri, nje ya punda katika kisiwa hicho kilichopo kilometa 341 kutoka Mombasa. Dk Timamy alimuagiza Mkuu wa Wilaya, Joseph Kanyiri, kukamata wakazi wanaokiuka amri ya kupeleka magari, pikipiki na baiskeli kwenye mji wa kihistoria wa Lamu.

Mji huo upo katika urithi wa dunia chini ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).

Agosti 2015 serikali ya Kaunti ya Lamu iliunda sheria ya kuondoa magari, pikipiki na baiskeli kwenye mji huo wa kale na badala yake kuamuru wanaotembea kwa miguu na punda pekee kuhudumu kwenye mji huo.

Akihutubia wakazi mjini Lamu, Dk Timamy alisema; “Lamu ni mji wa kihistoria, magari, baiskeli na pikipiki vinaharibu ukale wa hapa. Tumewahi kushuhudia mama aliyegongwa kwa baiskeli karibu apoteze uhai. Kila wakati mimi husema hatutaki magari, pikipiki wala baiskeli hapa mjini Lamu.

“Polisi wafanye kazi yao kwa kuwakamata wanaokiuka sheria hiyo. Ukitaka kutumia gari lako, itakubidi uvuke Mokowe au eneo lingine na wala si mjini Lamu,” alisema Dk Timamy na kusisitiza magari maalumu tu, yakiwemo ya serikali ndiyo yanayoruhusiwa, tena kwa vibali.

Wataalamu wengi huamini ya kwamba mji wa Lamu uliundwa katika Karne ya 14. Historia ya mji huo ambayo ni taarifa iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika Karne ya 16, inadai ya kwamba chanzo cha mji kilitokea wakati wa kufika kwa familia moja kutoka Shiraz (Uajemi) katika karne ya tatu baada ya Hijra iliyonunua kisiwa kutoka watu wa bara. Mji ulistawi kwenye biashara kati ya pwani la Afrika Mashariki na Bara Arabu pamoja na Uhindi.

Kilikuwa kituo kwa ajili ya majahazi.

BARAZA jipya la mawaziri nchini Burundi, lililoteuliwa na Rais mpya, ...

foto
Mwandishi: LAMU, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi