loader
Picha

Tanzania, Rwanda kupeana watalii

WAONGOZAJI watalii wa Tanzania na Rwanda, wameweka mikakati ya pamoja ya kuongeza idadi ya watalii katika nchi hizo, kwa kuhakikisha wanatangaza utalii wa pande zote kwa manufaa ya wote.

Katika ushirikiano huo, watalii watakaofika Tanzania watakuwa na fursa ya kwenda pia kutalii Rwanda kwa kuunganishwa na waongoza utalii wa Rwanda, huku watalii watakaokwenda Rwanda na kutaka kuona wanyama na utalii mwingine wataunganishwa nchini, kwani nchi hiyo haina wanyama zaidi ya sokwe.

Katibu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waongoza Watalii (TATO), Sirili Akko amesema, ushirikiano huo utazaa matunda kwa nchi zote mbili kwa kuongeza watalii, ambao walikuwa wakiishia nchi moja bila kwenda nyingine.

Amesema katika kuimarisha ushirikiano, kampuni 13 za utalii nchini zilikwenda Rwanda kwa wiki moja, wawakilishi wake wakitembelea vivutio mbalimbali vya utalii ili kuwa rahisi kuelezea watalii wanaofika Tanzania kutembelea nchini Rwanda.

Akko amesema waliamua taasisi hizo mbili zinazoongoza watalii, zisaidiane kushawishi watalii wa nchi moja kutembelea nyingine kujionea vivutio zaidi, hasa kwa vile hazipo katika moja ya nchi hizo.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi