loader
Picha

Ajali ndege ya Ethiopia itufumbue macho

TANZANIA inaungana na ndugu zake wa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Kimataifa, kuomboleza vifo vya abiria 149 na wafanyakazi wanane wa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka katika kiwanja cha ndege cha Bole jijini Addis Ababa ikienda Nairobi, Kenya.

Ajali hiyo imeacha simanzi kubwa kwa Kenya kupoteza raia wake 32, Uganda (1), Rwanda (1), Somalia (1), Sudan (1), Djibouti (1), Nigeria (1), Togo(1), Misri(6), Ethiopia (17), Msumbiji (1) huku nchi nyingine pia zikipoteza raia wake.

Tunaungana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais John Magufuli wa Tanzania, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Gutterez kutoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliofariki.

Tunaungana pia na wananchi wa Tanzania kuomboleza msiba huu mzito, ukizingatia kuwa wengi wa waliokufa katika ajali hiyo walikuwa wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Masuala ya Mazingira (UNEP) ulioanza Nairobi jana.

Ni katika muktadha huo, tunasema ajali hiyo siyo tu imeacha pigo kwa majirani zetu, Kenya, Uganda na nyingine za Afrika na mataifa mengine duniani kwa kupoteza raia wao, bali pia ni pigo katika harakati za kutunza mazingira.

Ndio maana tunasema, tumesikitishwa na kuhuzunishwa na vifo vya ndugu zetu hao waliokufa wakiwemo wasomi, wafanyabiashara, maofisa wa UN, serikali za nchi mbalimbali, wanafunzi na wananchi wa kawaida waliokuwa na matumaini kuendelea kuchangia maendeleo.

Wakati tukisubiri ripoti za wachunguzi wa ajali hiyo kutoka taasisi zinazohusika na usalama wa anga Ethiopia, zikisaidiana na zile za kimataifa, tunaomba ndugu, jamaa na marafiki wa ndugu waliokufa, wapokee salamu zetu za pole na kumshukuru Mungu kwa hayo wakiganga yajayo.

Hata hivyo, tunaomba ajali hii iwe fundisho kwa mamlaka zinazohusika na usafiri wa anga EAC na duniani kwa jumla, kuchukua hatua thabiti kuimarisha usalama wa usafiri wa anga, kuzuia ajali kama hizo kutokea tena kama si kupungua.

Ajali hii iwe fundisho kwa kampuni za ndege kama Ethiopian Airlines, mashirika ya EAC na mengineyo, kukagua kila mara mifumo ya usalama wa ndege zao.

Ni kweli ndege inaweza kupata ajali muda wowote kwa sababu imeundwa kama chombo kinachoongozwa na mifumo, hivyo kuweza kupata hitilafu. Hata hivyo, ukaguzi wa kila mara husaidia pia.

TAARIFA ya kwamba idadi ya vifo vya waendeshaji bodaboda kwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi