loader
Picha

Vipaumbele bajeti ya trilioni 33/-

MPANGO wa Maendeleo wa 2019/2020 umeweka vipaumbele vikubwa katika maeneo makubwa manne kwa lengo la kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.

Akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/2020 jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (pichani) alisema mpango huo unalenga kujenga viwanda vya kukuza uchumi na kujenga misingi ya uchumi wa viwanda.

Dk Mpango alisema Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 ni wa nne katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka, umezingatia kufikia azma ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Ilani ya CCM. Alisema vipaumbele vilivyoaminishwa katika Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17- 2020/21 unalenga kuhuisha eneo la ujenzi wa viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda.

Alisema miradi itakayotekelezwa katika eneo hilo, ni ile inayolenga kujenga viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini hususani kilimo, madini na gesi asilia.

“Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia, uanzishwaji na uendelezaji wa kanda maalumu za kiuchumi na kongane za viwanda, viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo, mifugo na uvugi, kuongeza thamani ya madini na usimamizi endelevyu wa rasilimali misitu,” amesema Dk Mpango.

Alisema eneo la kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu, miradi itakayotekelezwa inayolenga upatikanaji wa huduma za afya, elimu na ujuzi, upatikanaji wa chakula na lishe bora hudujma za maji safi na salama.

“Shughuli zitakazotiliwa mkazo ni pamoja na kugharamia utoaji wa elimu ya msingi bila ada, kupunguza vifo vya akinamama vinavyotokana na uzazi utekelezaji wa programu za maendeleo ya sekta ya elimu, ujenzi na ukarabati wa vyuo vya ufundi nchini na kuboresha huduma za maji vijijini,” alisema.

Kuhusu eneo la uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji, waziri alisema miradi itakayotekelezwa ni yenye lengo la kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu (reli, bandari, nishati, viwanja vya ndege na barabara).

“Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kufua umeme wa maji Rufiji (megawati 2,115), kuboresha Shirika la Ndege Tanzania, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge na kuendelea na utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara na uwekezaji.

“Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2019/20, umeweka msukumo katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza ikiwemo kupitia upya mfumo wa kitaasisi, kisera na kisheria pamoja na kanuni zake ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje katika kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.

Katika eneo la kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mpango, alisema miradi itakayotekelezwa ni ile inayolenga kuimarisha mfumo na taasisi za utekelezaji wa mpango, kuweka mfumo utakaowezesha upatikanaji wa uhakika wa raslimali fedha na kuweka vigezo vya upimaji wa mafanikio ya utekelezaji.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi