loader
Picha

Michezo ya kubahatisha yachangia bilioni 96/-

SEKTA ya michezo ya kubahatisha inakadiriwa kuchangia Sh bilioni 96 mwaka huu wa fedha, huku jitihada zikijieleza kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha mfumo wake unakuwa ni wa kielektroniki.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe alisema katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, sekta ilichangia Sh bilioni 78.

Alisema wamejipanga kuanzia Julai mwaka huu, kutakuwa na mfumo mmoja wa kielektroniki na wadau ambao ni kampuni za michezo ya kubahatisha, hivyo kuwa na uhakika wa takwimu sahihi za mapato ya serikali.

“Si kwamba hatuna uwezo wa kujua mapato ya serikali katika kampuni hizo, tuna uwezo huo na nguvu za kisheria, muhimu ni kwamba kwa kuwa na mfumo huo tutakuwa na uhakika pasi na shaka wa mapato yetu,”alisema.

Alisema kampuni mbalimbali za mchezo wa kubahatisha zimewekeza mamilioni ya shilingi, huku Watanzania takribani 20,000 wakiwa wamepata ajira za moja kwa moja kutoka kwenye kampuni ya zinazoendesha mchezo huo.

Akizungumzia hatua ya hivi karibuni ya kupiga marufuku utitiri wa matangazo hasa kupitia redio na televisheni, alisema ili watanzania wanufaike na michezo hiyo ni lazima iwe katika utaratibu.

Alisema kuwapo bodi maana yake ni kuhakikisha michezo hiyo inachezwa kwa kufuata sheria za nchi na kwa manufaa ya taifa, ikiwamo kuongeza pato na kuchangia ustawi wa jamii hususani kwa washindi katika michezo hiyo.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 4 ya mwaka 2003, ndiyo inayosimamia sekta ya michezo ya kubahatisha nchini. Iko chini ya Wizara ya Fedha na ni taasisi ya umma ambayo muundo wake uko kama yalivyo mashirika ya umma. Ina bodi ya wakurugenzi inayoteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango. Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wanateuliwa na rais.

WAKATI Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inakaribia mwishoni wababe na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi