loader
Picha

Taasisi za Serikali zachangamkia ushauri wa Mwanasheria Mkuu

MWANDISHI Mkuu wa Sheria, Sarah Barahomoka amesema hivi sasa kuna mwamko mkubwa serikalini, taasisi na jamii kupata ushauri au maoni ya kisheria kutoka Ofi si ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Hivi sasa kuna mwamko mkubwa wa kutaka kupata ushauri, maoni au ufafanuzi wa kisheria kutoka kwetu na hili ni jambo nzuri ingawa limetuongezea wingi wa kazi na majukumu,” alisema Barahomoka.

Alisema hayo katika mahojiano maalumu na kusisitiza kwamba mwamko huo unadhihirisha ni kwa namna gani wizara au taasisi zinataka kutoa uamuzi kwa kuzingatia matakwa ya kisheria na kufuata sheria.

“Hivi sasa hawathubutu (wizara/taasisi) kufanya kitu bila kupata maoni ya kisheria, wapo wanaotupigia simu au kuleta barua zao wakitaka ufafanuzi au maoni wanapokumbana na utata wakati wa kutekeleza sheria fulani, lakini pia ni kutaka kujiridhisha wanachotaka kukitolea maamuzi hakitazua malalamiko kutoka kwa jamii,” anasisitiza Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Aliongeza kusema mwamko huu pia unatokana na kwamba wananchi au jamii kwa ujumla kwa sasa imekuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya sheria na wanajua wapi pa kupata haki zao.

“Viwango vya uwajibikaji kwa watoa maamuzi vimeongezeka na hii ni kutokana na uelewa wa wananchi, kwa hiyo utaona wizara au taasisi ikiandaa nyaraka zake lazima wahakikishe Mwanasheria Mkuu anahusishwa kwa sababu ya kuelewa kwamba kuna kuwajibika Bungeni au kwa jamii pale mambo yatakavyo kuwa ndiyo sivyo,” alifafanua.

“Zamani mtu alikuwa anaweza kutoa uamuzi fulani na asiwajibishwe kwa sababu jamii haikuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya sheria, lakini sasa mazingira yamebadilika mno, uelewa ni mkubwa na wasomi waliohitimu sheria ni wengi na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa wa kuwasaidia wananchi kuhusu haki zao na masuala ya kisheria,” aliongeza.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi