loader
Picha

UVCCM wafufua chuo cha Ihemi

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekifufua Chuo cha Umoja wa Vijana Ihemi mkoani Iringa ili ‘kupika’ viongozi na wanachama waive kisiasa, kimaarifa na kiujuzi.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James alisema katika chuo hicho ambacho kilikuwa kikitumika kwa shughuli za chama na umoja huo, kwa muda kilisimama mafunzo, lakini kitaanza tena. Mara kitakapoanza kutoa mafunzo mwezi ujao, licha ya kutoa mafunzo kwa viongozi pia kitafungua milango kwa vijana wengine wanaotaka kupata elimu ya kisiasa, kiujuzi na maarifa, watapata fursa ya kusoma bila kulipa gharama zozote.

“Chuo cha Ihemi cha viongozi wa UVCCM kitakuwa kitovu cha maarifa na ujuzi ili kusaidia vijana wasiendeshe siasa kwa hisia, bali kwa utafiti na uhalisia,” alisema James. James alisema katika kuwapa maarifa na ujuzi vijana, chuo hicho pia kitatoa elimu ya kilimo, uvuvi na biashara ili kuwajengea uwezo wa kwenda kuanzisha na kuzalisha bidhaa mbalimbali katika maeneo yao.

Aliwataka vijana popote walipo nchini, kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo miradi ya kimkakati ili kushiriki katika miradi hiyo na kupata maendeleo. Alisema katika ziara waliyofanya katika maeneo mbalimbali nchini, walibaini vijana wapo tayari kufanya kazi hivyo akawaomba wakuu wa wilaya kuwatumia vijana ambao ni nguvukazi katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema jukumu la wakuu wa wilaya ni kuwatumia vijana hao ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika shughuli na huduma mbalimbali hasa kuwapa fursa ya kufanya kazi katika miradi inayopatikana katika maeneo yao. “Wakuu wa wilaya wanatakiwa kuhakikisha wanatumia vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika maeneo yao kwa kuwapa nafasi kushiriki katika miradi ya mashamba, madini, uvuvu na shughuli nyingine katika kuleta maendeleo,” alisema.

James pia vijana wenyewe wanatakiwa kutumia fursa zilizopo katika mazingira yao, kama uvuvi, kilimo, biashara au kwenye madini, waanze kuhangaika na kutafuta kazi katika maeneo mengine wakati wanakotoka kuna fursa.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi