loader
Picha

TLS yakiri utata usajili kwa njia ya mtandao

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimekiri kuna changamoto ya kutumia mfumo mpya wa usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA ) kwa njia ya mtandao kwa kuwa mawakili wengi hawajaujua vizuri ili kuwasaidia wateja wao ambao ni wafanyabiashara.

Mwanzoni mwa mwaka jana, Brela ilianzisha mfumo huo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao na kuacha kufanya usajili na huduma kwa njia ya karatasi. Wakili kutoka TLS, Benedict Ishabakaki alisema hayo wakati ujumbe wa TLS ulipokutana na Brela ili kujadiliana kuhusu mfumo huo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao ambao una mwaka mmoja sasa.

Ishabakaki alisema wao TLS kama wadau wakubwa wa mtandao huo ni muhimu kuutathmini mfumo huo ili iwe rahisi kuwashauri na kuwasaidia wateja wao ambao ni wafanyabiashara.

Pamoja na changamoto hiyo, alikiri kuwa mfumo huo ni mzuri kwa kuwa unarahisisha kazi na unahamasisha uwekezaji kutokana na uharaka tofauti na ilivyokuwa awali wakati wa kujaza kwenye karatasi. Alisema changamoto nyingine ni kwa baadhi ya wafanyakazi walioko Brela ambao hawana ushirikiano mzuri na wateja wao jambo ambalo uongozi umeahidi kushughulikia.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi alisema kwa kuwa mfumo huo mpya sasa una mwaka mmoja, wakala umeona ni vema kuwaita wadau mbalimbali ili kujadiliana nao kuhusu unavyofanya kazi na changamoto zake hivyo kwa kuanzia wameanza na hao mawakili.

“Tunataka kusikia kutoka kwa TLS wamepokea vipi mfumo huu mpya, kama ni kurekebisha turekebishe wapi na mafanikio ni yapi tuboreshe wapi zaidi,” alisema Kakwezi. Alisema baada ya TLS watakutana na wadau wengine wakiwemo Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Umoja wa Mabenki na Taasisi inayojihusisha na wafanyabiashara wadogo (Vibindo).

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi