loader
Picha

Nyota 5 Yanga kuwakosa Lipuli

KIKOSI cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo asubuhi kinatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 kwenda Iringa kukabiliana na Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, bila ya baadhi ya wachezaji wake nyota.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora keshokutwa. Katika msafara huo watakosekana nyota wake watano wanaoumwa ambao wamekuwa tegemeo na mhimili kwenye kikosi hicho kutokana na mchango wanaoutoa wakiwa uwanjani.

Akizungumza na gazeti hili Mratibu wa Kikosi hicho, Hafidhi Saleh alisema mipango yote ya maandalizi iko sawa kuwakabili wapinzani wao na wanakwenda kwa basi kuwakabili Lipuli.

“ Katika msafara wetu tutawakosa wachezaji wetu, Ibrahim Ajib, Juma Abdul, Ramadhan Kabwili, Andrew Dante, Abdallah Sahibua ambao wanaumwa kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa daktari wetu, hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi chetu,” alisema.

Saleh amesema, pamoja na kuwakosa wachezaji hao, lakini kikosi chao kamwe hakiwezi kutetereka kwani wana uhakika wa kuendeleza makali yao huko Iringa.

Yanga ambao hadi sasa wapo kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa hazina ya pointi 67 wanaenda kucheza mchezo huo wa 28 wakiwa na matarajio ya kupata ushindi ili kuhakikisha wanatimiza shabaha yao ya kutwaa taji hilo msimu huu.

Wanaenda kucheza na Lipuli wanaoshika nafasi ya tano kwenye msimamo huo kwa pointi 39, ambao kwenye michezo uliopita kwenye uwanja huo walitoka suluhu na Mbao FC.

Mbali na wachezaji, Yanga pia inakwenda Iringa bila kocha wao, Mwinyi Zahera ambaye amekwenda katika majukumu ya timu ya taifa ya Congo, ambaye yeye ni kocha msaidizi, huku Lipuli nao wakitarajia kumkosa kocha wao, Selemani Matola aliyefungiwa.

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi