loader
Picha

Nyota wa mabao hashangai kutoitwa Stars

KINARA wa mabao Ligi Kuu Bara, Salim Aiyee wa Mwadui hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars chini ya kocha Emmanuel Amunike, suala ambalo amekiri limezidi kumuongezea hasira na changamoto ya kufanya vizuri zaidi ili wakati mwingine ajumuishwe katika kikosi hicho.

Aiyee, ambaye ana mabao 15 dhidi ya wapinzani wake wa karibu; Meddie Kagere wa Simba na Heritier Makambo wa Yanga, ambao kila mmoja amefunga mara 12, tofauti ilivyotarajiwa na wengi mshambuliaji huyo hajajumuishwa katika kikosi hicho kinachojiandaa kucheza dhidi ya Uganda kuwania kushiriki michuano ya Afcon.

“Hapo awali sikuwahi kuitwa Stars kwa hiyo kwangu si kitu cha kushangaa sana ingawa kwa kasi na juhudi nilizonazo msimu huu wengi walitarajia itakuwa hivyo, pamoja na hayo naona bado nina nafasi ya kuitwa katika siku za usoni.

Stars ipo Kundi L katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 5 sawa na Lesotho iliyo nafasi ya tatu.

Kinara ni Uganda yenye pointi 13 wakati Cape Verde ikiwa ya mwisho na pointi zake nne. Stars itahitaji ushindi katika mchezo huo huku ikiombea Lesotho ifungwe na Cape Verde.

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi