loader
Picha

'Wachezaji Simba waandaliwe kisaikolojia'

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Azam FC, Juma Mwambusi amesema wachezaji wa Simba wawe watulivu na wasibabaike na presha kubwa watakayopata kutoka kwa mashabiki na viongozi, wakati watakapocheza dhidi ya AS Vita katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika Jumamosi.

Simba ambao hadi sasa wanashika mkia kwenye Kundi D wakiwa na pointi sita, wanaweza kufuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo endapo wataibuka na ushindi wowote katika mchezo huo dhidi ya klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo Simba itakuwa ikisaka kulipa kisasi baada ya kufungwa 5-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Congo.

Akizungumza na gazeti hili, Mwambusi alisema wachezaji wa Simba wanakabiliwa na mchezo mgumu mbele yao, ambao unashika hatma yao ya kufuzu kwa robo fainali au kutupwa nje ya michuano hiyo.

“Wachezaji wasibabaike na presha kutoka kwa mashabiki na viongozi, wanahitaji utulivu na kocha Patrick Ausseums anatakiwa awajenge kisaikolojia vizuri, naamini watafanya vizuri kwa kuwa walishakutana na timu hiyo na wanaijua licha ya kupoteza”, amesema Mwambusi.

Kocha huyo aliyetimuliwa Azam FC alisema hadi sasa kundi lao bado liko wazi na Simba wana nafasi kubwa na kufuzu endapo tu wataibuka na ushindi katika mchezo huo na hilo litawezekana endapo wachezaji watajengwa kisaikolojia kuelekea mchezo huo.

Hadi sasa kundi hilo linaongozwa na JS Saoura ya Algeria kwa pointi nane ikifuatia na Al Ahly na Vita ambao kila mmoja ina pointi saba, hivyo kama Simba atapata ushindi wa pointi atajihakikishia kutinga hatua inayofuata kwani atakuwa na pointi tisa, na kuungana na mshindi katika mchezo wa Al Ahly dhidi ya Saoura utakaopigwa siku

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi