loader
Picha

Watanzania kushindana riadha, kikapu Rwanda

TIMU ya Tanzania itakayoshiriki michezo ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ya Kanda ya Tano ya Afrika yatakayofanyika Kigali, Rwanda mwezi ujao, inatarajia kuondoka nchini Machi 31, imeelezwa.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema Tanzania katika michezo hiyo itapeleka wachezaji tisa na makocha wawili wa michezo ya riadha na mpira wa kikapu.

Alisema kuwa timu ya riadha ambayo itakuwa chini ya kocha Mwinga Mwanjala inaundwa na Regina Mpigachai (meta 800/1500), Amosi Charles (meta 400), Gaundencia Maneno (1500), Ester Martin (meta 3,000) na Francis Damas (meta 5,000).

Alisema kuwa kocha wa timu ya mpira wa kikapu ni Phineas Kahabi, wakati wachezaji ni Josephat Sanka, Charles Majombo, Daud Maiga na Ally Abdallah.

Amesema, timu ya mpira wa kikapu itashiriki mchezo wa wachezaji watatu watatu, huku ikiwa na mchezaji mmoja wa akiba.

Amesema michezo hiyo itaanza jijini Kigali Aprili 2-4 wakati timu hiyo ya Tanzania inatarajia kurejea nchini kati ya Aprili 7 na 8.

Amesema, michezo hiyo inafanyika Rwanda kwa ajili ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu nusu milioni yaliyotokana na mapigano ya kikabila nchini humo.

Bayi alisema kuwa jumla ya nchi 10 zinatarajia kushiriki michezo hiyo, ambazo ni wenyeji Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Eritrea, Sudan, Somalia na Misri.

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi