loader
Picha

Vikosi SMZ vyatamba Ligi Kuu Zanzibar

TIMU tatu za vikosi vya SMZ juzi vilitoka kidedea katika michezo yao ya Ligi Kuu ya Zanzibar iliyopigwa kwenye viwanja tofauti.

Timu hizo ni KVZ ambayo iliifunga Mwenge mabao 2-1, JKU iliyoisambaratisha Jamhuri kwa bao 1-0 na Mafunzo iliyoipeleka puta Mbuyuni kwa kuikandika mabao 3-0.

KVZ na JKU zilishuka katika Uwanja wa Amaan saa 8:00 mcahna na saa 10:00 Mafunzo ilishuka katika dimba la Mao Dze Tung saa 10:00 Jioni.

Katika mchezo uliowakutanisha KVZ na Mwenge, mabao yake yalifungwa na Ayoub Lipati dakika ya nane na Abdul Yussuf dakika ya 26 wakati bao la kufutia machozi la Mwenge liliwekwa kimiani na na Jumanne Alawi katika dakika ya 52. Kwa upande wa timu ya JKU iliyoshuka uwanjani hapo saa 10:00 za jioni, bao lake la pekee liliwekwa kimiyani na Mbarouk Chande katika dakika ya 46.

Licha ya kushinda kwa vikosi hivyo pia vimerudi tena katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kwanza ili kuwa mabingwa baada ya kuingia katika hatua ya tatu bora kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Aidha, huko kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani saa 8:00 mchana, Selem ilionja machungu kwa kufungwa mabao 2-0 na Mlandege, huku wa saa 10:00 jioni Polisi ikafungwa na Chipukizi kwa idadi kama hiyo ya magoli.

Chipukizi kwa ushindi huo imefikisha pointi 23 na kuwa katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo wakati Polisi bado wapo katika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 35.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi hiyo, KMKM inaongoza ikiwa na pointi 55 wakifuatiwa na KVZ ambao nao wana pointi 55, JKU inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 wakati Malindi inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 53.

Nafasi ya tano kwa sasa inashikiliwa na Mafunzo wenye pointi 50 wakati Mlandege wapo nafasi ya sita wakiwa na pointi 48, huku Zimamoto wanashika nafasi ya saba wakiwa na pointi zao 45 na Chuoni ipo nafasi ya nane pointi 38.

Kwa mujibu wa msimamo huo bado timu sita za Pemba zipo katika mstari mwekundu ikiwemo Mwenge yenye pointi 20 nafasi ya 14, New Star 20 nafasi ya 15, Mbuyuni nafasi ya 16 pointi 16, Hard Rock wa 17 pointi 14, Opec wa 18 pointi 14 na Kizimbani inashika mkia nafasi ya 19.

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi