loader
Picha

Halmashauri zakumbushwa kukarabati majosho

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezikumbusha halmashauri nchini ambazo hazijakarabati majosho kadiri ya maagizo aliyotoa akiwa Chato, mkoani Geita.

Waziri Mpina amekumbusha agizo hilo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutathmini uogeshaji mifugo limefikia wapi tangu lizinduliwe Novemba mwaka jana.

Mpina amesema kwa halmashauri ambazo hazijatekeleza hilo, anakusudia kuwaandikia barua ya kusudio la kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa halmashauri zilizoshidwa kutekeleza agizo la kukarabati majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji.

Alisema katika uzinduzi uliofanyika Chato, alitoa maagizo manne kwa halmashauri zote nchini, likiwemo la kukarabati majosho, lakini baadhi ya halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza.

"Pia nilisema majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha mifugo yao kwa urahisi lakini kwa mkoa wa Dodoma ikiwemo Mpwapwa haijakarabati josho hata moja sawa na asilimia. Pia alisema agizo lingine ni kuunda kamati za majosho kote nchini zitakazo ratibu zoezi la uogeshaji wa mifugo.

"Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazorudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini," amesema.

"Na itakapofika Julai mwaka huu, halmashauri zote ambazo zimeshidwa kutekeleza hayo yote nitawanyang'anya mamlaka ya kukusanya mapato yote yatokanayo na bidhaa za mifugo," amesema Waziri Mpina.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dk Hezron Nonga alisema tangu zoezi la uogeshaji lizinduliwe nchini asilimia 56 ya mifugo yote nchini imeogeshwa kwa muda wa miezi mitatu.

Dk Nonga alisema mifugo walioogeshwa ni ng'ombe milioni 19.9, mbuzi milioni 8.8, kondoo milioin 2.88, punda 224 na mbwa 202,900. Pia Dk Nonga alisema, lengo la mkakati huo ni kuboresha mifugo kwa kuwakinga na magonjwa ambayo husababishwa na kupe, papasi na mbu.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Mpwapwa

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi