loader
Picha

Chakula cha Ufaransa kuliwa Dar

UBALOZI wa Ufaransa nchini umeandaa hafla ya sanaa ya kutayarisha, kupika na kula chakula cha nchi hiyo.

Hafla hiyo intarajiwa kufanyika Machi 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ushirikiano kati ya nchi hizo katika utamaduni.

Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, Ufaransa ina lengo la kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na katika utamaduni.

"Toka mwaka 2015 tukio hili limefanyika duniani kila Machi 21 kusherehekea na kutambua utamaduni, kwa hapa Tanzania tumeanza hapa Dar es Salaam, tunatumaini miaka ijayo tutafanya na katika miji mingine, ushirikiano wetu na Tanzania ni katika mambo mbalimbali," amesema Balozi Clavier.

Amesema nchi hiyo pia imeongeza misaada yake zaidi ya mara mbili ya iliyotolewa mwaka uliopita na kwamba inapenda kuona Tanzania inafikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda mwaka 2025.

Balozi Clavier amesema, siku hiyo inayotambulika kama 'gastronomy day' kutakuwa na vyakula vitakavyoandaliwa hapa nchini na wapishi wataalamu kutoka Ufaransa.

Amesema, pia kutakuwa na vinywaji ukiwemo mvinyo, shampeni na burudani kutoka Ufaransa.

Ameipongeza Tanzania kwa jitihada za kudumisha tamaduni zake hasa katika upande wa vyakula.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi