loader
Picha

Manusura mauaji ya Kibiti aomba msaada

MANUSURA wa matukio ya mauaji ya viongozi na wananchi katika Wilaya ya Kibiti, Michael Buchayandi (32) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rondo wilayani hapo anaomba msaada wa matibabu ya macho baada ya kupata upofu kutokana na jeraha la risasi na jicho jingine kupigwa na kitu kizito na watu wasiojulikana.

Michael ambaye alinusurika katika matukio ya mauaji ya viongozi wa serikali za mtaa katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani miaka miwili iliyopita, alidhaniwa amekufa hivyo kuchanganywa na marehemu wengine wawili ambao ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangwi na Mtendaji wa Kata ya Mchukwi.

Akisimulia tukio hilo, jana mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambako aliongozana na mkewe, Selina Mponyi (30), Michael alisema amenusurika kwa uwezo wa Mungu ila amepata upofu. Hata hivyo, akielezea kwa ufupi tukio hilo, mkewe alisema baada ya mumewe kuchukuliwa na watu hao na kusogezwa vichakani walisikia mlio wa risasi na wao kujua ameshauawa na ndipo baada ya muda tena wakasikia milio ya risasi jirani.

Alisema walipoingia ndani ya nyumba yao hawakuwakudhuru watu wengine isipokuwa walimpiga mumewe na kitu kizito kwenye jicho moja na kisha kumchukua na kutokomea naye gizani hadi kesho yake wanavijiji walipoanza kumtafuta na kumkuta akiwa taabani amefungwa pamoja na maiti za viongozi wengine ambao ni Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangwi.

“Namshukuru Mungu, walidhani mume wangu kafa ila hakufa risasi waliyompiga iliharibu jicho lote la kulia na hili la kushoto lilipoteza uoni kutokana na kipigo cha rungu, sasa amebaki kipofu, ila tumeambiwa hospitalini anaweza kuona hili jicho moja ila kinachohitajika ni fedha,” alisema Selina.

Kwa undani wa habari hii soma Makala katika Jarida Jamii ndani ya Gazeti hili siku ya Jumatatu (18/3/2019) wiki ijayo.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi