loader
Picha

Kesi ya akina Mbowe kusikilizwa mfululizo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga siku mbili mfululizo kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko jana walifika mahakamani hapo wakitokea uraiani baada ya kukaa gerezani kwa miezi minne. Kesi hiyo ambayo imepangwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amepanga kusikiliza shauri hilo kwa siku mbili mfululizo.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai kuwa kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo jana kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Simba aliieleza mahakama kuwa, amepewa maelekezo jana asubuhi kuwa shauri hilo limepangwa mbele yake kwa kuwa Hakimu aliyekuwa akisikiliza awali amebadilishiwa kituo cha kazi.

Kesi hiyo awali likuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbald Mashauri ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu. Hakimu alieleza kuwa kesi hiyo itaendelea pale ilipoishia na aliutaka upande wa mashitaka kuwasomea upya washitakiwa mashitaka yanayowakabili ambayo waliyakana.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Wakili Simon aliiomba mahakama irejee uwamuzi wa mahakama kuu kwamba shauri hilo lisikilizwe haraka iwezekanavyo. Wankyo alimuomba na hakimu apange tarehe ya kuanza kusikiliza kesi hiyo ili walete mashahidi. Wakili wa utetezi, Profesa Abdalah Safari aliiomba mahakama ipange tarehe za usikilizwaji kulingana na kalenda yao kwa kuwa wana kesi zingine katika mahakama kuu na wameshalipwa. Hata hivyo, Hakimu Simba alikataa ombi hilo kwa kuwa kesi hiyo inawakili wengine wa utetezi hivyo wanaweza kumwakilishwa.

“Hatuwezi kupanga tarehe kulingana na kalenda zenu nyie mawakili, kama wewe hautakuwepo mawakili wenzio watakuwakilisha, sheria inaelekeza kesi zisikilizwe mapema ili ziishe,” alieleza Hakimu Simba. Baada ya maelezo hayo, Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 28 na 29 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mashahidi wa upande wa mashitaka.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine ni Katibu Mkuu Chadema Taifa, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Chadema Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, John Heche na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Wanadaiwa Februari 16, mwaka jana katika viwanja vya Buibui na Mwananyamala Kinondoni wakiwa walikusanyika na azma ya pamoja, waliitekeleza kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa aman Pia wanadaiwa kuwa Februari 16, mwaka jana katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.

Inadaiwa kugoma huko kulipelekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwilin na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi. Katika mashitaka mengine ya uchochezi wa uasi linamkabili Mbowe, anadaiwa Februari 16, mwaka jana katika maeneo Dar es Salaam, alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau kwa upande wa raia wa Tanzania dhidi ya mamlaka halali. Bulaya anadaiwa Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam alïtenda kosa la kukaidi amri halaĺi ya tamko la Jeshi la Polisi.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi