loader
Picha

Mamilioni kutibu figo Muhimbili, BMH yaokolewa

SERIKALI ilikuwa ikitumia kati ya Sh milioni 80 hadi 100 kusafisha figo na kupandikiza figo India, lakini sasa inatumia Sh milioni 21 tu.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulilef “Zamani kabla hatujaanza kutoa huduma za kusafisha damu na kupandikiza figo nchini tulikuwa tunatumia kati ya Sh milioni 80 hadi 100 kumtibu mgonjwa mmoja India lakini sasa tunatumia Sh milioni 21,” Dk Ndugulile alisema.

Alitoa takwimu hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Siku ya Figo Duniani na kuwataka Watanzania kubadili mfumo wa maisha kujikinga na maradhi ya figo. Alisema wagonjwa 42 wamepandikiziwa figo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (38) na Hospitali ya Benjamini Mkapa (4) Dodoma na wote bado wapo hai na wanaendelea vizuri.

“Wakati tunatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya matibabu ya mgonjwa wa figo, kwa mgonjwa wa malaria tunatumia chini ya Sh 2,000, kwa hiyo tupambane na magonjwa ya figo,” alisema. Alisema ugonjwa wa figo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza yanayogharimu fedha nyingi kuyatibu kuliko magonjwa yanayoambukiza. Dk Ndugulile alitahadharisha wananchi kutumia dawa za kutuliza maumivu bila ya ushauri wa daktari kwani zinasababisha ugonjwa wa figo.

Alisema siku za hivi karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa figo tofauti na zamani ambapo unywaji wa dawa za kutuliza maumivu kiholela umekuwa ukichangia. Alisema serikali imeweka mashine za kusafisha figo hospitali za kitaifa na kikanda ambapo mpango sasa ni kuweka mashine hizo kwenye hospitali zote za rufaa ili kutoa wigo mpana kwa wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi.

Daktari Bingwa wa Figo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Onesmo Kisanga alisema asilimia 10 ya watu duniani wana matatizo sugu ya figo na Tanzania asilimia 6.8 wana usugu huo. Alisema wananchi ni vema wakajihadhari na matumizi holela ya dawa za kupunguza maumivu diclofenac za kichina na kienyeji.

Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dk Grace Maghembe aliwataka Watanzania kufanya mazoezi kuepuka magonjwa yasiyoambukiza. Alisema kusafisha figo kila siku mtu hulipia Sh 250,000 ambapo kwa mwezi anatakiwa kusafishwa mara nne sawa na sh milioni moja. Dalili za ugonjwa huo ni kuvimba, tumbo, uso na miguu kujaa maji. Dk Ndugulile alisema mgonjwa akishafikia hatua ya kuvimba mwili inakuwa ni hatua za mwisho za ugonjwa huo.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi