loader
Picha

Zanzibar kujenga Hospitali kama Mloganzila

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inatarajia kujenga hospitali kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kubeba vitanda 1,000 ili kutoa huduma na kufundishia watalaam wa afya.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ali Abdulla alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila kujifunza na kupata uzoefu juu ya uendeshaji wa hospitali hiyo. Alisema ziara hiyo imefanyika kuokana na agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein karibuni.

Dk Shein aliwataka watendaji wa wizara hiyo kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila kupata uzoefu wa uendeshaji wake katika tiba na mafunzo kwa wataalamu walioko kwenye mazoezi kwa njia ya vitendo. Asha alisema ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa mithili ya Hospitali ya Mloganzila utaanza katika mwaka huu wa fedha 2019/2020.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri. Alisema kwa sasa wananchi walio wengi wanategemea Hospitali ya Mnazi Mmoja yenye vitanda 776 iliyozidiwa wingi wa wagonjwa.

“Tumekuja kujifunza kwenu kwa kuwa mna uzoefu mkubwa wa kuendesha hospitali kubwa kama hii na sisi tunahitaji kujipanga, kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha kutoka kwenu ili hospitali yetu ikikamilika tuweze kuiendesha vizuri kama wenzetu mnafanya” alisema Asha.

Hospitali hiyo itajengwa Binguni wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja kwa awamu kulingana na rasilimali zinavyopatikana. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof Lawrence Museru ameahidi kutoa ushirikiano na uzoefu wa kila aina ili lengo la ujenzi wa hospitali hiyo lifanikiwe.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi