loader
Picha

Masauni akerwa na kusuasua ujenzi nyumba za Magereza

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (pichani) ameeleza kusikitishwa na kusuasua kwa ujenzi wa nyumba za Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam ambazo Rais John Magufuli alitoa Sh bilioni 10 ili kufanikisha ujenzi huo.

Kutokana na hali hiyo amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ili kubaini chanzo cha kusuasua kwa ujenzi huo ambao ukikamilika utawezesha kuhifadhi familia 320 za askari Magereza.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi, Naibu Waziri Masauni alisema kasi ya ujenzi wa mradi huo hairidhishi na umechukua muda mrefu kukamilika huku changamoto ya makazi kwa askari, ikiwa ni kubwa na Wakala wa Majengo(TBA) waliopewa fedha hizo kujenga wakitoa majibu yasiyoeleweka “Namuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani akae na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wabaini nini tatizo linalosababisha mradi huu kusuasua na tayari Rais Magufuli ameshatoa kiasi hicho cha fedha na zote zimeshatumika na mradi bado haujakamilika.

“Dhamira ya serikali ni kuhakikisha tunajenga nyumba za askari nchi nzima, tushaanza katika baadhi ya mikoa huku Tanzania Bara na Visiwani ikiwemo Dodoma, Arusha na Pemba. Askari wetu kuishi uraiani inazorotesha utendaji wao,” aliongeza Masauni.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza,Uwesu Ngarama alisema changamoto ya makazi kwa askari ni kubwa huku akiweka wazi juhudi wanazofanya kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa kutatua changamoto hiyo.

“Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike amezindua kampeni jijini Dodoma ambayo inahusisha ujenzi wa nyumba za maofisa na askari kwa njia ya ubunifu au kujitolea ambayo ni maelekezo kwa mikoa yote ikiwa ni moja ya njia ya kutatua matatizo ya makazi kwa askari,” alisema Kamishna Ngarama.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi