loader
Picha

Wateja kampuni ya simu kugawana faida ya bil. 2.1/-

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inatarajia kugawa faida ya Sh bilioni 2.1 kwa wateja wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.

Faida itokanayo na Airtel Money ni fedha ambazo Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka, kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku.

Kiwango hicho cha faida kwa kila salio la mteja kinatolewa pia kulingana na jinsi mteja anavyotumia huduma ya Airtel Money, mteja atatumiwa faida yake kwenye akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kuamua kuzitoa au kuzitumia kwa matumizi yoyote ikiwemo kulipia bili mbalimbali kama vile za Dawasco na LUKU. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam jana na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Fidelis Kaijage wakati wa kutangaza kuanza kugawa faida hiyo.

“Faida itokanayo na matumizi ya Airtel Money itagawiwa kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wote nchini ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi sita iliyopita kati ya Aprili na Septemba 2018”alisema.

Hii ni mara ya saba kwa Airtel kutoa faida kwa wateja wake wote wa Airtel Money tangu 2015. Mpaka sasa Sh bilioni 16 zimetolewa kama faida kwa wateja na mawakala wote nchini. Naye Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Airtel, Jackson Mmbando alisema lengo la kugawa fedha hizo ni kuendelea kuwafikia wateja ambao ni muhimu kwenye biashara ya fedha.

“Wateja wetu tunawahakikishia huduma ya papo kwa hapo za kutoa pesa ni bure na vilevile ukiwa na Airtel Money bado utaweza kupata mikopo rahisi kutoka Airtel TIMIZA Mkopo ili kufanikisha jambo lolote la dharura, ipo huduma ya kujiwekezea akiba kwa ajili ya matumizi ya baadaye kupitia TIMIZA Vikoba,” alisema na kuongeza kuwa Airtel Money ina mawakala zaidi ya 60,000 nchini kote. Kulingana na utafiti wa TCRA wa hivi karibuni wa Desemba 2018, inaonyesha kuwa huduma ya Airtel Money imekua kwa haraka na kufikia asilimia 25.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi