loader
Picha

Zahera atangaza vita

VINARA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Yanga wamesema watapambana na wekundu wa Msimbazi Simba katika harakati za kuwania taji la Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi usiku kwenye kambi yao Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema walipoanza msimu hawakuwa na malengo yoyote wakijua wanaweza kuwa katika nafasi ya tano au sita, lakini baada ya kuona mwenendo wao ni mzuri sasa anatangaza rasmi lazima wapiganie taji. “Hatuwezi kujificha hasa ikizingatia kwamba tulifanya vizuri mzunguko wa kwanza na wa pili pia, tumeanza vyema, natangaza rasmi kwamba tutapambana na Simba kuwania taji la Ligi Kuu,” alisema.

Zahera alisema mwenendo wao ulikuwa mzuri isipokuwa walianza kupoteza baadhi ya mechi kwa madai ya waamuzi kushindwa kuchezesha kwa haki. Alisema wanachokiangalia katika michezo iliyobaki ni kuhakikisha wanafanya vizuri mpaka mwisho na kuchukua taji hilo sambamba na kubeba Kombe la Shirikisho la Azam (FA). Yanga kwa sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 67 katika michezo 27 kiasi cha kujiamini na kuona kuwa ina nafasi ya kupigania taji hilo linaloshikiliwa na Simba. Wanafuatiwa na Azam yenye pointi 56 na Simba pointi 51 lakini ikiwa na michezo saba kibindoni.

Kilio Bodi ya ligi Kocha huyo alilalamikia ratiba ya Ligi Kuu kuwabana katika mechi zijazo ikionesha kutakiwa kucheza kila baada ya siku tatu katika mikoa iliyoko mbali na kwamba licha ya kupeleka barua kuomba kuliangalia hilo, Bodi hiyo imewakatilia na kuweka msimamo kuwa ni lazima wacheze. “Mchezaji akicheza mechi anatakiwa apumzike saa 72 kwa sababu mwili unakuwa umechoka ili mwili uweze kurejea katika hali ya kawaida, lakini sasa unakuta safari ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine mpaka ufike haupumziki wala kupata muda wa kufanya mazoezi,” alisema na kutolea mfano wanatakiwa wacheze Mwanza kisha waanze safari ya Mtwara. Alisema kwa ratiba hiyo ngumu hata kubeba kombe lenyewe itakuwa ni kazi kubwa.

Wachezaji wafundwa Katika mkutano huo wa waandishi ulihudhuriwa na wachezaji, viongozi na wadau wa klabu wakiwafunda wachezaji kujitambua na kujipanga kimaisha. Kwa upande wa kocha aliwataka wachezaji kujua kuwa kuna maisha baada ya mpira hivyo, wanapaswa kujipanga wakati wowote kama baba wa familia. Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay aliwataka wachezaji kujiandaa na maisha kwa kuhakikisha wanawekeza kibiashara au hata kimasomo ili mwisho wa siku wakiachana na soka wawe na kitu kingine cha kufanya.

KOCHA wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi