loader
Picha

Tunahitaji mikakati mipya kukabili ukatili

NI ukweli usiofi chika kwamba pamoja na kuwapo kwa sheria mbalimbali, sera na mipango mizuri ya kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya aina zote za ukatili, vitendo vya ukatili vimeendelea kujitokeza maeneo mengi nchini.

Ni kweli kuwa pamoja na nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi zilizosaini na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda yenye lengo la kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili, bado kiwango cha ukatili kinatishia akili na upole wa wakazi wa taifa hili.

Kutokana na mazingira hayo tunapenda kuunga mkono kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Utu wa Mtoto ( CDF), Koshuma Mtengeti kwamba kwa hali ilivyo sasa tunahitaji mikakati maalumu kuikabili.

Na katika kuungana kwake tunapongeza juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo za kuandaa kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto linalotarajiwa kufanyika Machi 22 hadi 23 mwaka huu.

Tunaamini kwamba Kongamano hilo ambalo litawakutanisha watafiti, asasi za kiraia, wanataaluma, viongozi wa dini, wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari litakuja na mwarobaini utakaokomesha kabisa vitendo hivyo.

Tunaweza kusema kwamba ukatili unaofanywa dhidi ya watoto katika mazingira ya majumbani kwetu, kwa ndugu zetu, katika huduma za jamii ni kielelezo tosha kwamba wakati umefika wa kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuinasua jamii yetu katika dhiki hii iliyopo.

Tunazungumza hivyo kwa kuwa pamoja na kampeni zote zinazofanyika dhidi ya mimba za utotoni, mimba hizo zinaongezeka; pamoja na kuwapo kwa waraka maalumu wa namna ya kutoa adhabu kwa watoto hasa adhabu ya fimbo bado walimu hawazingatii maelekezo na pamoja na kifungo kinachosubiri bado watu wanakeketa watoto wao.

Kwa kuangalia ukweli kwamba sera zipo sheria zipo na adhabu zipo lakini matukio kama haya ya kudhalilisha watoto na wanawake yanaendelea, hivyo jawabu la msingi ni kuunganisha mawazo na kuona kwa namna gani adhabu zilizopo sasa kisheria na hata sera hazitusaidii kukomesha tatizo hili na tufanyeje kuweza kulitatua.

Tunaamini kupitia kongamano hilo litakalowahusisha wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi, tutaweza kujadiliana kuhusu hali halisi ya ukatili pamoja namna ya kuanzisha na kuimarisha mikakati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kutengeneza taifa linalozingatia sheria.

Kwa kuwa kongamano hilo litaangazia mada kuu sita ambazo ni pamoja na hali ya ukatili kwa watoto katika familia na mashuleni, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji, mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ukeketaji, malezi katika ulimwengu wa kisasa, ukatili wa kingono katika taasisi za elimu ya juu, ukatili dhidi ya watoto kwenye mitandao na namna yakuwapatia msaada wathirika wa vitendo vya ukatili, tunaamini kwamba shauri hilo litaangaliwa kwa makini na kwa mapana yake na kuja na majibu yenye kutoa uelekeo bora zaidi na wenye uhakika katika vita kukabili ukatili kwa wanawake na watoto.

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi