loader
Picha

Kiwanda cha bia hatarini kubomolewa

WIZARA za Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zinatarajia kukutana ili kutatua mgogoro wa umiliki wa eneo kilipojengwa kiwanda cha Bia cha Serengeti mjini Moshi (SBL) ambacho kipo hatarini kubomolewa.

Tayari Shirika hodhi la Reli (RAHCO) limeweka alama ya X kutaka kubomolewa kwa sehemu ya eneo la kiwanda hicho pamoja na makazi yawananchi wanaozunguka eneo hilo kata ya Bomambuzi katika manispaa ya Moshi.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya ameyasema hayo mara baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya viwanda,biashara na mazingira kutembelea kiwanda hicho kufahamuchangamoto zake kabla ya wizara hizo kukutana.

Manyanya alisema serikali imesema inaunga mkono juhudi kubwa za uwekezaji zilizofanyika kiwandani hapo na kukitambua kiwanda hicho kama miongoni mwa viwanda ambavyo ni walipaji wakubwa wa kodi nchini.

“Uwekezaji uliofanyika hapa ni mkubwa niwatoe hofu wawekezaji wetu kwamba serikali inatambua mchango wao, ardhi kwa ajili ya reli ipo,tutatoa maamuzi, huyu ni mwekezaji makini tungependa kuona akiendelea kuwepo,”alisema.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Sadiq, alisema kamati imezungumza na wataalamu wa Manispaa ya Moshi na SBL ambapo- Bunge limehakikishiwa mazungumzo na taasisi za serikali kuhusu mgogorohuo yanaendelea.

Amesema katika mgogoro huo, serikali ya wilaya na mkoa unaihakikishiamenejimenti ya SBL kwamba mgogoro huu umekwisha lakini hadi sasahawana barua yoyote kuonesha mgogoro huo umemalizika jambo ambalo linawatia mashaka juu ya uwekezaji wao.

“SBL na wananchi wameelezwa wasiwe na wasiwasi, mgogoro huu utakwisha, sisi kama Bunge tunazingatia mambo matatu, Kuitambua kesi mahakamani, Barua ya kubomoa na Kutokuwapo kwa barua ya kuonesha mgogoro umekwisha…kisha tutatoa ushauri,” amesema.

Amesema mgogoro huo unahitaji utatuzi wa haraka kwani unashirikisha wawekezaji wawili, wa ndani na nje ya nchi na kwamba, lengo ni kuhakikisha wawekezaji hawakatishwi tamaa lakini pia bunge linaunga mkono juhudi za serikali kuelekea Tanzania ya viwanda.

Amesema kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo, Dk Anna Mghwira, wanaunga mkono uwekezaji kiwandani hapo na kutaka majadiliano kufanyika kwani pia reli hiyo inapita umbali wa takribani Km moja kutoka kilipo kiwanda cha SBL.

Mapema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha amesema wana imani na kamati ya Bunge na kwamba ujio wao unadhihirisha jinsi serikali inavyoweza kushirikiana na sekta binafsi katika kutatua changamoto zilizopo na kuona sekta hiyo inakuwa.

“Kama ukibomoa kiwanda hiki utapoteza ajira ya maelfu ya Watanzania, fursa kwa wakulima wanaosambaza nafaka kama mahindi, shayiri na mtama, tuna imani na kamati katika kutatua mgogoro huu,” amesema.

WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi