loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Kenyatta amwokoa mwenye ufaulu wa juu

MSOMI wa chuo kikuu aliyekuwa na ufaulu mzuri wa daraja la kwanza, lakini akaishia kukosa kazi na kubaki kijijini akilea wadogo zake, amepata bahati ya mtende baada ya kujikuta akipata ajira kwa agizo la Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta alichukua hatua hiyo baada ya kusoma taarifa za msomi huyo, Ruth Jemutai Rono (27) kupitia vyombo vya habari. Ruth kutoka Lelbatai, Baringo Kati na ambaye ni mchumi aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Chuka mwaka 2015, tayari ameshaanza katika Tume ya Udhibiti Nishati Kenya yenye ofisi zake Upper Hill, jijini Nairobi.

Amemshukuru Rais Kenyatta kwa kumfanyia muujiza ambao hakuutarajia maishani mwake, akisema alishakata tamaa ya kupata ajira. “Naishukuru Ofisi ya Rais, hasa Rais Kenyatta. Alituma ujumbe kupitia maofisa wake na walinileta Nairobi kuja kuanza kazi. Sina uzoefu lakini namhakikishia Rais Kenyatta kwamba sitamwangusha, nitawatumikia Wakenya kwa nguvu zangu zote.

Nashukuru maombi yangu ya kupata ajira yamejibiwa,” anasema Ruth 918000018 aliyekiri kupitia maisha magumu akiwa kijijini. Mzaliwa huyo wa kwanza katika familia ya watoto wanane, ndiye aliyetegemewa kutunza wadogo zake, wakiwemo wawili wa kike ambao ni walemavu. Anasema mama yako alirejea kwao miaka mitatu iliyopita baada ya kuugua, huku baba akiwa hao, lakini amedaiwa kuwa ameitekeleza familia kwa kushinda katika klabu za pombe.

BARAZA jipya la mawaziri nchini Burundi, lililoteuliwa na Rais mpya, ...

foto
Mwandishi: BARINGO, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi