loader
Picha

Samia kufungua Jukwaa la Biashara Lindi

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kufungua jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji mkoani Lindi, ambalo limeanza rasmi leo mkoani humo.

Hiyo ni mara ya pili jukwaa hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu. Jukwaa la nane lililofanyika mkoani Tabora, lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Jukwaa la tisa Lindi, linafanyika katika hoteli ya Sea View likitanguliwa na maonesho yatakayofanyika siku tatu mfululizo na siku ya ufunguzi kesho yanayotarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 350.

Ratiba iliyotolewa na Kamati ya maandalizi ya jukwaa hilo inayoshirikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kampuni ya TSN, inaonesha mawaziri wanatarajia kushiriki jukwaa hilo pia.

Mmojawao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe; anayetarajiwa kuwa Mwenyekiti wa jukwaa.

Jukwaa hilo ni la nane kuandaliwa na TSN kwa kushirikiana na mikoa. Majukwaa yaliyopita yalifanyika mikoa ya Simiyu, Mwanza, Tanga, Shinyanga, Zanzibar, Arusha, Tabora na Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema mkoa huo uko tayari kulipokea jukwaa hilo na wanatarajia kupata matokeo mazuri ya maendeleo ya mkoa huo kupitia jukwaa hilo.

“Kwa muda mrefu tulikuwa tunataka mkoa wetu usikike, sasa hii ni fursa adhimu kwetu. Tunatarajia makubwa baada ya jukwaa hili, fursa zetu za uwekezaji na biashara zitajulikana Tanzania nzima na dunia kote,” alisisitiza.

Anasema washiriki mbalimbali wa mkoa huo, watajitokeza kwa wingi. Miongoni mwao ni wajasiriamali kutoka halmashauri zote sita za mkoa huo watakaonesha bidhaa wakishirikiana na taasisi na mashirika ya umma na binafsi.

Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah alisema jana maandalizi kwa TSN yanakwenda vizuri katika kuhakikisha jukwaa hilo linakwenda vizuri kama lilivyopangwa.

Alisema ana uhakika jukwaa hilo litaacha alama kwa maendeleo ya mkoa wa Lindi kama ilivyokuwa katika mikoa mingine lilikofanyika.

Aidha, aliipongeza timu ya waandishi wa habari wa TSN ambayo imekuwa Lindi kwa wiki tatu kwa kazi nzuri kutangaza fursa zinazopatikana huko baada ya kupita wilaya moja hadi nyingine na kuandaa toleo maalumu litakalotoka kesho.

Kwa mujibu wa ratiba, wengine wanaotarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo ni wakuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa

WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Lindi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi