loader
Picha

Taasisi 300, Halmashauri 180 waunganishwa GePG

BENKI ya NMB imeunganisha taasisi zaidi ya 300 nchini na halmashauri 180 katika mfumo ulipaji na kukusanya mapato serikalini (GePG).

Hayo yalielezwa na Meneja Uendelezaji Biashara wa NMB makao makuu, Masato Wasira alipotoa mada katika mkutano wa wadau wa maji nchini uliofanyika Dodoma.

Wasira alisema NMB imefanikiwa kuunganisha taasisi hizo mbalimbali zaidi ya 300 zikiwemo halmashauri 180 kupitia mfumo wa GePG.

Alisema mamlaka za maji 22, idara tano za maji, na bodi za mabonde ya maji saba zimeunganishwa katika mfumo huo wa malipo.

Wasira alisema kupitia mfumo GePG, wateja wanaweza kulipia miamala ya ankara za maji kupitia mitandao ya simu za mkononi au matawi ya Benki ya NMB 220 yaliyoenea nchini nzima.

Amesema wateja hao wanaweza kulipia ankara zao za maji kupitia mawakala wa NMB zaidi ya 6000, Internet banking na kupitia NMB mobile.

Aidha alisema benki hiyo ina wateja zaidi ya milioni 2.5 na imetoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 3,000 na inapatikana wilaya zote.

Amesema inatoa huduma kwa wafanyabiashara, wakulima, kampuni, taasisi na serikalini. Kupitia utoaji huduma bora unaotolewa na benki hiyo, imetajwa na taasisi ya Kimataifa ya Euromoney ni benki bora Tanzania mara sita.

WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi