loader
Dstv Habarileo  Mobile
Magufuli apewa tuzo ukuzaji Kiswahili

Magufuli apewa tuzo ukuzaji Kiswahili

CHAMA cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Tanzania (CHAWAKITA) kimetoa Tuzo ya Heshima kwa Rais John Magufuli kutokana na mchango wake mkubwa wa kuthamini na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

Tuzo hiyo kwa Rais imetolewa na chama hicho na kupokewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kwa niaba ya Rais Magufuli. Alipokea tuzo hiyo juzi mjini Morogoro wakati akifunga kongamano la 11 la kitaifa la Chawakita lililofanyika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.

Kongamano hilo la siku nne lilibeba kaulimbiu inayosema, “Kiswahili, Hazina ya Afrika kwa Maendeleo Endelevu” na kuandaliwa kwa tuzo kwa washindi wa uandishi wa vitabu vya hadithi fupi pamoja na ya heshima ambayo aliyotunukiwa Rais Magufuli kutokana na anavyoenzi na kukitilia maanani Kiswahili.

Pia tuzo nyingine ya heshima ilitolewa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na mchango mkubwa wa wizara hiyo katika kusimamia na kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini. Naibu Waziri Shonza baada ya kupokea tuzo hizo, aliupongeza uongozi wa chama hicho kwa kutambua umuhimu wa mchango wa Rais katika kukithamini na kukuza Kiswahili ambaye kwa sasa amekuwa ni balozi namba moja wa Kiswahili Tanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5e6d95d7badf14791e42e0c669c371f7.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi