loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali mbioni kupanga bei ya dawa za binadamu

SERIKALI iko mbioni kupanga bei ya dawa zote za binadamu, zinazouzwa kwenye maduka ya dawa ili kuondoa changamoto ya utoaji huduma na kudhibiti ubora.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania, Elizabeth Shekalaghe wakati akiwasilisha mada ya utendaji kazi wa baraza hilo kwa waandishi wa habari.

Shekalaghe alisema watoa huduma ya maduka ya dawa, wengi wao wamefanya huduma hiyo kuwa biashara zaidi na kwamba ili kudhibiti ubora, serikali iko mbioni kupanga bei za dawa zote ili kuondoa changamoto iliyopo sasa ambayo kila duka lina bei yake ya dawa. “Tunafikiri njia bora zaidi ya kuboresha huduma za uuzaji dawa kwenye maduka ya dawa kwa kupanga bei mwongozo ili kudhibiti ubora wa huduma,” alisema Shekalaghe.

Alisema hivi sasa kuna jumla ya maduka ya dawa 1,683 yaliyosajiliwa kwa ngazi ya maduka ya famasi nchi nzima na kati ya hayo, zaidi ya maduka 800 yako jijini Dar es Salaam. Aidha, yale yaliyosajiliwa kwa ngazi ya Maduka ya Dawa Muhimu (ADDO), yapo zaidi ya 13,000 nchi nzima na kwamba ipo haja ya sasa ya kuyasajili upya ili kuyaondoa yale yasikidhi vigezo kwa mujibu wa sheria.

“Tunataka pia tusajili upya maduka yote ya dawa kuanzia yale yanayouza dawa za jumla hadi dawa muhimu, lengo ni kuhakikisha yanafuata kanuni na sheria kwa sababu lengo letu kuu ni kulinda afya ya huduma za dawa zitolewazo,” alisema Shekalaghe. Katika hatua nyingine, alisema mtoa huduma ya dawa katika duka la dawa ngazi ya famasi, anapaswa kuwa mfamasia na haruhusiwi kuuza dawa za cheti cha daktari kwa wateja wasio na cheti hicho kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume na kanuni na iwapo dawa italeta madhara sio rahisi kumfuatilia mgonjwa.

Hivyo alitaka watoa huduma wote kwenye maduka hayo, kuzingatia kanuni na sheria na wale wayakaobainika kutoa dawa hizo bila cheti watachukuliwa hatua za kisheria. Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa baraza hilo, Grace Malange alisema hadi sasa nchi ina wafamasia waliosajiliwa 1,863, na idadi ya wafamasia imekuwa ikiongezeka kwa miaka ya sasa, baada ya kuwepo na vyuo zaidi ya kimoja vinavyotoa elimu ya fani hiyo, ukilinganisha na miaka ya nyuma.

WADAU mbalimbali kutoka asasi za kiraia wamekutana kujadili ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi