loader
Picha

Karume, Nyerere watukumbushe umoja

JANA Watanzania Bara na Visiwani waliungana kukumbuka siku ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Shehe Abeid Amani Karume.

Karume aliuawa siku kama ya jana mwaka 1972 na ameendelea kukumbukwa kama mmoja wa waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais John Magufuli ziarani wilayani Mbinga, mkoa wa Ruvuma alitaka wananchi kuendelea kuenzi kazi nzuri iliyofanywa na Karume na pia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Tunaungana na Watanzania wote na wananchi wa Unguja na Pemba katika kumbukizi ya Karume tukienzi mambo yote mazuri aliyoacha.

Moja ya mambo mengi ni ujenzi wa nyumba za kisasa kwa ajili ya wananchi maskini maarufu kama maghorofa ya Michenzani, umoja, amani na ushirikiano na muungano imara wa Tanzania.

Karume na Nyerere wanaingia katika vitabu vya historia kama viongozi waliounganisha nchi zao, Tanganyika na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye nguvu duniani.

Ndio maana tunaungana na Rais Magufuli kutaka wananchi waendelee kuwaenzi Nyerere na Karume kila kumbukizi zao zinapowadia.

Ni matumaini yetu kuwa, kumbukizi ya Karume jana itaendelea kuwa dira ya viongozi wa Zanzibar chini ya Rais Dk Ali Mohammed Shein na Rais wa Muungano, Dk Magufuli, kuendeleza mazuri ambayo waasisi walituachia.

Chini ya Nyerere na Karume Tanzania ilipiga hatua kubwa za maendeleo na imeendelea hivyo hata baada ya kifo cha Karume hivyo ni vyema dhamira na malengo ya waasisi yakaendelezwa.

Pamoja na matatizo madogo madogo wengine wakiziita kero za muungano, bado Muungano wa Tanzania umeendelea kuwa mfano wa kuigwa Afrika na duniani kwani ni wa pekee.

Ni wa pekee kwa sababu umeshuhudia viongozi wa Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakiendelea kushirikiana kwa maslahi ya nchi.

Itakuwa jambo jema kama kumbukizi ya jana ya Karume itawakumbusha wananchi wa pande zote mbili za muungano, umuhimu wa kuishi ndoto za waasisi hao ili wananchi wapate maendeleo.

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Monduli

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi