loader
Picha

Mimba kwenye umri mdogo mateso kwa watoto

MARIAM (si jina halisi) ni binti wa miaka 16 mkazi wa Kijiji cha Berege katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Alipata ujauzito akiwa na miaka 14 wakati huo akisoma Shule ya Msingi Berege na kwa sasa mtoto wake ana mwaka moja na miezi saba.

Mariam ni miongoni mwa mabinti 30 waliojifungua wakiwa na umri mdogo wanaopatiwa mafunzo ya afya ya uzazi, stadi za maisha, uongozi na ujasiriamali na shirika lisilokuwa la kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF).

“Nilianza kujihusisha na mapenzi na kijana pale kijijini nikiwa na miaka 14. Sikujua kama ninaweza kupata mimba, lakini nikawa nikihisi mabadiliko kwenye mwili maana nilikuwa nachoka sana, hata nikikimbia kidogo tu,” anasema.

“Sijui walimu walinigunduaje kwani tumbo lilikuwa halionekani kabisa, ila nilikuwa nashindwa kukimbia mchakamchaka… hata mwalimu akiingia darasani kufundisha nilikuwa nalala, walimu wakapata shaka na hali yangu, nikaenda kupimwa hospitali nikagundulika nina ujauzito wa miezi mitano,” anasema.

Hata hivyo, baadhi ya walimu walitaka niendelee na masomo, lakini wakanisisitiza nisimuambie mama jambo hilo.Mimba huwa ina kawaida ya kuchosha nadhani kwangu ilikuwa ikinichosha sana, naingiwa na uvivu hata wa kuamka, niko darasani mwalimu anafundisha nakuwa siwezi hata kumuangalia kule mbele naona bora nilale tu darasani,” anasema Mama anaambiwa ujauzito Binti huyo anasema ukifika wakati akawa anashindwa hata kwenda shule kwani akiamka anajisikia mwili umechoka na hauna nguvu.

Anasema kuna wakati alimaliza mwezi mzima bila kwenda shule hali iliyoufanya Uongozi wa Shule kumtumia barua ukitaka afike shule akiwa na mzazi wake. “Nilikwenda shule na mama ndipo alipoambiwa wamegundua kuwa mimi ni mjamzito,” anasema Mariam.

Anasema tangu wakati huo, mama yake aligeuka kuwa mbogo kwani alikuwa akimpiga kila mara wakati mwingine bila hata sababu ya msingi. Anasema nyumba wanayoishi ni ya vyumba vitatu na amekuwa akiishi hapo na mama yake mzazi, ‘baba wa kufikia’ na wadogo zake.

“Mimi mama alisema baba yangu alimuacha akiwa na ujauzito kwa hiyo mimi nimelelewa na mama na nimekuja kumfahamu baba yangu nikiwa darasa la tano alikuja hapa kijijini” anasema.

Anasema baba yake ni Mzaramo mwenyeji wa Dar es Salaam na alifika kijijini hapo miaka mitatu iliyopita ndipo mama yake akamuambia kuwa huyo ndiye baba yake mzazi.

“Akanipa namba ya simu sasa tuna mawasiliano na baba yangu, nikawa kama nina shida ya daftari, nguo zimechanika ukipiga simu ukimwambia una shida anatuma kama ni Sh 20,000 au Sh 10,000 kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali,” anasema.

Anasema hapo kijijini, anaishi na baba wa kufikia ambaye aliwakuta tayari wakiwa kwenye nyumba ambayo alijenga mama yao.

“Nilipopata ujauzito huyu baba mdogo alikuwa mkali sana, alisema nisipotaja mimba ni ya nani, nihame hapo nyumbani. Kwa vile nilijua nimefanya mapenzi na nani nikamtaja kijana niliyekuwa nikijihusisha nae kimapenzi, Mike (sio jina lake halisi),” anasema binti huyo.

Anasema baada ya kugundua kuwa alikuwa anatafutwa kwa kuhuma za kumsababishia ujauzito, kijana huyo alikimbia, ingawa inasemekana yupo Arusha na mara kadhaa wamekuwa wakiwasiliana.

“Mike alimuona mtoto wakati akiwa mdogo, aliporudi na kuonekana kijijini akaanza kutafutwa tena, ikabidi aondoke tena tangu 2017 hadi leo sijamuona zaidi ya kusikia sauti yake kwenye simu,” anasema.

Anasema Mama wa Mike, alimtaka Mariam ahamie nyumbani kwake ili Mike arudi nyumbani na kutoa mahari, lakini mama mzazi wa Mariam akakataa suala hilo.

Maisha magumu

“Tangu nigundulike kuwa mjamzito, maisha yamekuwa magumu sana kwangu; yaani tangu nimejifungua mpaka sasa baba mdogo amekuwa akinitukana sana na hata sasa akikuona, utasikia anamuambia mama anipige; anasema ‘huyu angekuwa mtoto wangu namng’ata hadi sehemu za siri,” anasema.

Anasema siku moja alikwenda kuomba maji kwa mama mkwe wake (Mama Mike) kwa ajili ya kupikia, lakini jambo hilo lilileta ugomvi mkubwa. Hata hivyo siku iliyofuata baba yake mdogo alirudi na kutaka asongewe ugali na aliposema kuwa maji hakuna alianza kutukana.

“Akaanza kunigombeza ilipofika usiku akasema toto lako hilo (mwanangu) nikilinyanyasa utafurahi, akamshika mtoto mkono akaanza kuunyonga mtoto akaanza kulia nikaenda kumbeba nikakimbilia kwa dada yangu.”

“Nilikaa mpaka saa nane za usiku nikarudi nyumbani nikakuta mama akiwa nje ananisubiri aliponiona akaniambia ingia ndani nenda ukalale,” anasema

Anaongeza: “Maisha sio shwari baba mdogo hanitaki nyumbani wakati alipokuja aliikuta hiyo nyumba tumeshajenga na anakaa nyumba ya mama yangu.”

Anasema mwanaume huyo alianza kuishi na mama yake mwaka 2016 na hawajabahatika kupata mtoto na mama yake japo mama yake ana watoto wengine sita aliozaa na mwanaume mwingine.

Anasema malengo yake ni kufanya biashara ndogo ili aweze kumtunza mtoto wake. “Sasa hivi nina nguruwe mmoja mwenye mimba ninamiini wakiongezeka watanipa mtaji wa biashara,” anasema.

Msaada wa CDF CDF hutoa mafunzo hayo kwa ufadhili wa shirika la FORWARD-UK, pia Ufadhili wa Ubalozi wa Uholanzi pamoja na ubalozi wa Uswidi nchini Tanzania.

Mariam ni miongoni wa wasichana 25 waliopewa mafunzo ya ujasiriamali na mtaji wa kuanza ufugaji.

Yeye alifuga nguruwe na aliuza mmoja kwa Sh 110,000 fedha iliyomsaidia kwa mahitaji mbalimbali na kuweka akiba.

“Lakini sasa kuna shida nyingine pale nyumbani, baba na mama wanasema yule nguruwe ni wao kwa vile namfugia pale nyumbani maana natumia ardhi yao, ndio sasa nimetoa taarifa ili suala hilo lishughulikiwe,” anasema binti huyo.

Anasema uzazi katika umri mdogo umekuwa mtihani mkubwa na mgumu kwake kutokana na umri wake kuwa mdogo.

“Natakiwa kupambana ili nitoke katika hali hii, natakiwa kuwa na biashara au ufugaji utakaoniinua kiuchumi ili nimlee mtoto wangu na maisha yangu yaendelee kwa amani tofauti na sasa,” anasema.

Mafunzo ya stadi za maisha Stella Msambwa (20), ni miongoni mwa mabinti walio kwenye mafunzo hayo ya stadi za maisha.

Anasema alimaliza Kidato cha Nne Mwaka 2015 katika Shule ya Sekondari ya Pwaga, lakini hakufaulu kuendela na masomo.

“Nilibaki kijijini, nilijifungua Agosti 2016 na mwanaume aliyenipa ujauzito anaishi huko huko kijijini, lakini hana uwezo wa kulea mtoto, wazazi wangu ndio wananilea mimi na mtoto wangu,” anasema.

Anasema kupitia CDF wamepewa mafunzo mbalimbali yanayomsaidia kujitambua na kujiamini na hata namna ujasiriamali unavyoza kumsaidia kufikia malengo anayojiwekea kimaisha.

“Nilipenda niwe mwalimu, lakini ndoto zangu hazikutimia na sasa naelekeza nguvu zote kwenye ujasiriamali kwa vile sina uwezo tena wa kurudi shuleni,” anasema.

Anasema Februari mwaka huu, CDF kwa ufadhili wa shirika la FORWARD-UK, waliwafundisha ujasiriamali wa kutengeneza sabuni ili kuweza kujipatia kipato.

Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF)- Dodoma, Evans Rwamuhuru anasema wanafanya kila linalowezekana kuwasaidia mabinti hao kurejea katika njia ya kujitegemea.

Anasema mafunzo ya stadi za maisha na uongozi kwa wasichana zaidi ya 30 waliopata mimba katika umri mdogo, wa kata nne za Pwaga, Berege, Kibakwe na Mpwapwa Mjini wilayani Mpwapwa yanayofanyika chini ya ufadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania ni njia kuelekea ukombozi wa mabinti hao. Rwamuhuru anasema uwepo wa klabu za wasichana shuleni, pia umesaidia kuibua matukio mbalimbali ya ukatili kwani awali wanafunzi walikuwa hawasemi.

“Katika shule za msingi na sekondari 16 tunazofanya nao kazi tumetengeneza klabu za wasichana. Kila klabu ina wasichana 30 wanaofundishwa mambo mbalimbali yakiwamo haki za watoto na hata mifumo ya ulinzi…”

“Pia tunawasaidia kutambua kuwa ukatili sio haki yao na hawapaswi kukalia kimya aina yoyote ya ukatili. Lengo kuu ni kuwajengea ujasiri na uthubutu ili waweze kusema hapana juu ya matendo yote ya ukatili,” anasema.

Wasichana 60 walio nje ya shule waliopata mimba kwenye umri mdogo wapo katika vikundi vya watu 15 wanaofundishwa stadi za maisha, ujasiriamali na elimu ya afya ya uzazi.

Rwamuhuru anasema mafunzo hayo yamesaidia wasichana wa shule waliokuwa wakifanyiwa ukatili ukiwamo wa kingono kutoka kwa wanafunzi wenzao na watu wazima, kuutambua ukatili na kuthubutu kutoa taarifa katika mifumo ya ulinzi iliyopo karibu nao.

“Tukifundisha watoto na wao wanakwenda kufundisha watoto wengine juu ya

RIPOTI inayotolewa na jopo la kiserikali la kimataifa (IPCC) mara ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi