loader
Picha

Waziri SMZ aipongeza TTCL

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Sira Ubwa Mamboya, amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kutoa huduma bora za mawasiliano na usimamizi wa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano nchini.

Dk Mamboya alitoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam jana baada ya ziara yake katika Shirika la Mawasiliano Tanzania, kutembelea miundombinu na mitambo ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.

Katika salamu zake, waziri huyo alipongeza utendaji wa TTCL mpya ambayo inafanya juhudi kubwa za kuliimarisha shirika na huduma zake na kuonesha kufurahishwa na utaratibu wa shirika hilo kutoa ajira kwa kuzingatia pande zote za Muungano hali inayoimarisha udugu na uhusiano mwema.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba aliwashukuru viongozi wakuu wa SMZ kwa uongozi wao thabiti unaodumisha Muungano na kustawisha ushirikiano unaoiwezesha TTCL kutimiza vyema majukumu yake katika ofisi zake zote Tanzania Visiwani ambako inaihudumia serikali, taasisi za umma na sekta binafsi.

“Tunapopata ugeni kama huu, tunafarijika sana kwani kupitia tukio hili, uhusiano mwema wa kindugu baina ya pande mbili za Muungano unaimarishwa, Aidha, tunabadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kujenga mtazamo wa pamoja wa namna bora zaidi ya kuwahudumia wananchi wetu,” alisema Kindamba.

Shirika la Mawasiliano Tanzania lilizaliwa Februari Mosi, 2018, kwa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Namba 12 ya Mwaka 2017.

Kuundwa upya kwa shirika hili la TTCL ni matokeo ya kukamilika kwa mchakato wa kutunga sheria uliopitia katika hatua zake zote ikiwemo kuridhiwa na Bunge na hatimaye kupata idhini ya Rais, Novemba 28, 2017.

Huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano zinazosimamiwa na kuendeshwa na TTCL zimeiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano katika ukanda wa kiuchumi wa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kutokana na kuwa na mfumo mzuri kukusanya kodi kwa kutumia mfumo maalumu wa kielektroniki

WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi