loader
Picha

Semina elekezi muhimu kwa viongozi

MTIZAMO uliochukuliwa na Kituo cha Uwekezaji (TIC), Kanda ya Kaskazini ya kuweka utaratibu wa kutoa semina elekezi kwa viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuhusu masuala ya uwekezaji ili kuboresha ufanisi na kufungua fursa mpya za uwekezaji, ni mtizamo chanya na wa kuigwa.

Tunasema ni chanya kwa maendeleo ya nchi katika suala zima la uwekezaji na hasa tunapoelekea katika nchi ya viwanda.

Viwanda vinahitaji uwekezaji kuanzia mitaji midogo, ya kati hadi mikubwa. Ili nchi iweze kutimiza malengo yake katika hili, viongozi wote, wawe wa kuchuguliwa au kuteuliwa ni lazima waandaliwe, waive na wawe tayari kwenda na mtazamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa mujibu wa Meneja wa TIC wa kanda hiyo, David Riganda, hatua hiyo ni maazimio ya wakuu wa taasisi za umma ambao wanahusika moja kwa moja kufanikisha azma ya serikali katika uwekezaji.

Riganda akataja taasisi zinazohusika katika semina hiyo kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), maofisa biashara, uhamiaji, idara ya kazi, Shirika la Umeme (Tanesco) na idara ya ardhi.

Pia akasema viongozi watakaohusika na semina kuwa ni pamoja na wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, wakuu wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wabunge na madiwani, mada ikiwa ni kusaidia sekta ya uwekezaji.

Tunawapongeza viongozi wa Kanda ya Kaskazini kwa mtazamo huo ambao tunashauri, kanda nyingine nao waige mfano huo.

Ni kutokana na semina elekezi ambazo kwazo zinalenga kuimarisha watendaji wote katika maeneo husika, malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia hadi taifa yatafanikiwa.

Riganda anasema wameamua kuwashirikisha wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri na vyama vya ushirika ili kuainisha maeneo ya ardhi yaliyotengwa kwa ajili uwekezaji na kurahisisha huduma hiyo pale inapohitajika.

Hiyo dhana ya ushirikishwaji wa watendaji kufanikisha azma ya serikali ndiyo iwe dira kwa kanda zote. Tunaamini, kupitia semina hizi ambazo zinawahusisha watendaji, zikifanyika kwa nchi nzima, kutaleta mabadiliko chanya ambayo ndiyo yanayohitajika kwa hivi sasa.

Muda mwingi umepotea kwa watendaji kukaa na kujifungia maofisini, jambo ambalo limetufikisha hapa.

Viongozi wote waliopewa mamlaka wawe ni wakuchaguliwa au kuteuliwa ni lazima waje na mbinu mpya ya kuwezesha azma ya serikali kutimia kwa asilimia kubwa.

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi