loader
Picha

Watendaji msikwaze wawekezaji

RAIS John Magufuli amewataka mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi kumpa majina ya watendaji wa Serikali wanaowazungusha wawekezaji wanaotaka kuwekeza Tanzania kutoka nchi mbalimbali wanazoziwakilisha.

Ametoa kauli hiyo juzi mkoani Njombe wakati akizindua kiwanda cha kuchakata chai cha Kampuni ya Unilever kikiwa ni muungano wa kampuni za Uingereza na Ufaransa.

Rais Magufuli alisema moja ya changamoto alizoelezwa na Balozi wa Uingereza nchini, Balozi Sarah Cooke zinayopata wawekezaji wa Uingereza nchini ni usumbufu wa watendaji. Tunaungana na Rais Magufuli kueleza jinsi tunavyokerwa na watendaji wenye urasimu mkubwa katika idara mbalimbali za Serikali.

Urasimu unaofanywa na watendaji hao siyo ytu kwamba unakwamisha maendeleo ya wananchi bali unaikosesha serikali kodi kutoka viwandani.

Ni kwa kutambua hilo, tunasema tunakerwa na urasimu huo na kuomba watendaji wanaohusika kujisahihisha na kusaidia wawekezaji haraka.

Rais Magufuli alisema, asilimia tano ya kodi inayokusanywa nchini inatokana na kampuni za Uingereza zilizowekeza hapa ikiwemo Unilever.

Ni matumaini yetu watendaji walioguswa na kauli ya Rais Magufuli watabadilika na kuacha urasimu kwa nia ya kuharakisha maendeleo.

Ni muhimu wakabadilika ili kwenda na kasi ya Rais Magufuli kuleta maendeleo hasa ya viwanda kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. Kwa wawekezaji kutoka Uingereza na mataifa mengine tunaomba waendelee kuja kuwekeza na kuamini kauli ya Raia Magufuli kuwaenzi.

Ni matarajio yetu kuwa wawakilishi, mabalozi wa nchi za nje wataendelea kuhamasisha raia wao kuja kuwekeza katika ujenzi wa viwanda na maeneo mengine ya uvunaji raslimali zetu.

Tanzania ina sifa ya kujaliwa madini ya kila aina kuanzia dhahabu, Tanzanite, almasi na mengine, raslimali za misitu na pia utaliii. Ni matarajio yetu kuwa fursa hizo zitaendelea kuwavutia wawekezaji kutoka nje na hivyo kuchangia kukua haraka kwa uchumi wetu.

Tunaomba kila mtu kwa nafasi yake aawape wawekezaji kila aina ya ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii wanapoajiriwa kukuza uchumi.

Tunawashukuru wawekezaji walioko katika maeneo mbalimbali na kuomba wengine zaidi waje huku tukimpongeza Rais Magufuli kwa hatua nzuri anazochukua kukuza uchumi wetu.

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi