loader
Picha

KARIA AIHOFIA KENYA AFCON

RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kazi ipo kubwa kuwazuia Kenya kwenye mechi za fainali za kombe la mataifa Afrika, Afcon hatua ya makundi.

Katika droo iliyopangwa mjini Cairo, Misri na Shirikisho la soka Afrika, CAF juzi, Tanzania, Taifa Stars imepangwa kundi C pamoja na jirani zake Kenya, Senegal na Algeria.

Kwa nyakati tofauti Stars imeshacheza mara kadhaa za timu hizo katika mechi za kufuzu na haikuwa na matokeo mazuri sana. Stars mara ya mwisho ilicheza na Senegal mwaka 2009 na kufungwa 1-0, mwaka 2018 ilicheza na Algeria na kufungwa mabao 4-1 na ilitoka sare ya bao 1-1 na Kenya mwaka 2016.

Akizungumzia droo hiyo, Karia alisema, kazi kubwa itakuwa kwa Kenya kwa vile ni jirani na wote wanafahamiana aina yao ya soka. “Kenya na sisi tunafahamiana, ndio itakuwa kazi kubwa lakini hizo timu nyingine ni za kawaida, tutajipanga tu kuzishinda,” alisema.

Michuano hiyo imepangwa kuanza Juni 20 hadi Julai 19 na kwa mujibu wa ratiba, itaanza kete yake ya kwanza dhidi ya Senegal kabla ya kucheza na Algeria na kumaliza na Kenya.

Tanzania imefuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 tangu ilipofuzu mwaka 1980 ilipofanyika Lagos, Niger

SHIRIKA la Utangazaji la Tanzania (TBC), limeombwa kuangalia uwezekano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi