loader
Picha

China yafungua ubalozi Dodoma

KATIKA kuitikia hatua ya serikali kuhamia Dodoma, tayari China imefungua ubalozi mdogo mjini Dodoma, huku wakipongeza juhudi za Tanzania katika kupambana na rushwa na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha, Juni mwaka huu, Tanzania inatarajia kuanza safari za ndege kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam hadi mjini Guangzhou, China, lengo likiwa ni kuinua biashara na utalii katika nchi hizo mbili.

Akizungumza jijini hapa, Balozi wa China, Wang Ke alisema nchi yake imeamua kufungua ubalozi mdogo ikiwa ni kuitikia mwito wa serikali ya kuhamia Dodoma.

“Mwaka jana wakati wa hafla ya mabalozi, Rais John Magufuli alikabidhi hati za viwanja, ikiwa ni njia ya kuzialika nchi zetu kuhamia Dodoma, China tumeona umuhimu wa hilo, hivyo tumeamua kufungua ubalozi mdogo hapa Dodoma ambao pamoja na mambo mengine utatumika kuratibu ujenzi wa balozi hapa.

Aidha, Ke aliipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli kwa kupambana na rushwa na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Aidha, Ke ameishauri serikali ya Tanzania kutumia fursa ya kijiografia ya mji wa Dodoma katika kuimarisha uhusiano uliopo na kupiga hatua kwenye maendeleo ya kijamii na uchumi.

Aidha Ke alisema China imeialika Tanzania kushiriki katika majukwaa ya kibiashara, ikiwamo maonesho ya kimataifa ya mazao ya bustani yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Jukwaa la biashara la China-Afrika litafanyika Juni mwaka huu katika mji wa Changsha na maonesho makubwa ya China International Import Expo yatakayofanyika Novemba mwaka huu jijini Shanghai.

China ni nchi yenye uwekezaji mkubwa Tanzania ikiwa na miradi ya uwekezaji 723 yenye thamani ya dola bilioni 5.9 (Sh bilioni 13), ukizalisha ajira 87,126.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alisema Tanzania na China imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na kuwa uanzishwaji wa safari ya ndege hautasaidia Tanzania pekee katika kuimarisha utalii na biashara lakini pia bara la Afrika.

Pia Profesa Kabundi aliipongeza China kwa hatua yake ya kufungua ubalozi wake jijini Dodoma na alisema serikali ipo tayari kutoa msaada.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi