loader
Picha

Waandishi TSN washinda tuzo

KAMPUNI ya magazeti ya serikali (TSN) imeendelea kutesa baada ya waandishi wake wawili kushinda kwa mara nyingine tuzo za uandishi wa habari zinazohusu masuala ya watoto zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Waandishi hao ni Anne Rhobi wa Daily News aliyekuwa mshindi wa jumla katika kundi la waandishi wa habari waliojikita katika uandishi wa habari za watoto na Sifa Lubasi wa HabariLeo kutoka mkoani Dodoma Washindi kutoka vyombo vingine vya habari ni Anold Jovin kutoka Redio Kwazera mkoani Kagera na Mwanza ni Kiembe wa ABM FM Radio ya Dodoma.

Wengine ni Lilian Lugakingira (Nipashe na EATV ) Kagera, Suleyman Abeid (Majira) mkoani Shinyanga, Tumaini Msowoya na Rehema Matowo (Mwananchi).

Akizungumza wakati akikabidhi tuzo hizo, Mkuu wa mawasiliano, utetezi na uhusiano wa Unicef, Manisha Mishra alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Jukwaa la Wahariri katika kuwawezesha waandishi wa habari kuihabarisha jamii kuhusiana na ukatili wanaotendewa watoto katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tunatambua kwamba waandishi wa habari ni watu pekee wa kupaza sauti na kufichua yanayotendeka kuhusu watoto kwa hivyo Unicef tutaendelea kushirikiana na jukwaa la wahariri kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa ufanisi,” alisema Mishra.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Nevile Meena alisema mwakani watahakikisha wanaongeza idadi ya maeneo ya kushindanisha ili kupanua wigo wa ushiriki kwa waandishi wengi zaidi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alivitaka vyombo vya habari nchini kutambua wajibu wao wa kuendelea kuzipa kipaumbele habari zinazohusu masuala ya watoto na kufichua vitendo vyote vya ukatili wanavyotendewa ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo hivyo.

Balile alisema iwapo vyombo vya habari nchini vitajenga utamaduni wa kutoa kipaumbele kwa habari za watoto ni wazi serikali na wadau wengine wa watoto wataweza kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha mtoto wa Tanzania analindwa na kupata haki zake za msingi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari,Tanga

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi