loader
Picha

Wasomi UDOM waonya EPA

WASOMI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wameishauri serikali ya Tanzania isiharakishe kusaini Mkataba wa Ushirikiano ya Kiuchumi (EPA) na Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa kuwa nchi hizo hazilingani kiuchumi.

Ushauri huo wa wasomi wa Udom unaenda sambamba na wa Bunge ambalo liliishauri serikali ya Tanzania kujipa muda zaidi kabla ya kusaini mkataba huo wa EPA.

Ushauri huo wa wanazouni wa Udom ulitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya nne ambaye kwa sasa ni Mhadhiri wa Udom, Dk Cyril Chami wakati wa mdahalo wa wazi wa wanazuoni kujadili kwa nini nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania zisisaini makubaliano ya EPA.

Hadi sasa nchi za Afrika Mashariki zilizosaini mkataba huo ni Kenya na Rwanda, lakini Uganda, Burundi, Sudan Kusini na Tanzania hazijasaini mkataba huo wa ushirikiano wa EPA na Umoja wa Ulaya.

Dk Chami amesema hakuna ulinganifu wowote wa kiuchumi unaoshawishi nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kusaini mkataba huo na nchi za Ulaya kwa sababu mkataba huo utakuja kuziua nchi hizo kiuchumi.

Amesema Jumuiya ya nchi za Ulaya inayoundwa na nchi takribani 28 ambazo huchangia kwenye uchumi wa dunia asilimia 28 na pato la mwananchi mmoja mmoja wa jumuia hiyo kwa mwaka ni kiasi cha dola za Marekani 43,000 huku nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki zikichangia asilimia 0.24 ya uchumi wa dunia.

“Pato la mwananchi mmoja mmoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki ni dola za Marekani 918 kwa mwaka sasa unataka hawa watu wawili washirikiane kiuchumi? Ni sawa na mtu kama Goliath umwambie ashirikiane na mtoto mdogo kushindana nguvu,” amesema Chami.

Alisema mkataba huo wa EPA ni ukoloni mamboleo ambao unataka kuja kuitawala Afrika kwa njia nyingine na kuitaka Tanzania kujipa muda mrefu wa kutafakari athari za kusaini mkataba huo kabla ya kuingia rasmi.

Aidha, alibainisha kuwa mkataba huo utaziua nchi za Afrika Mashariki (EAC) kiuchumi hususani Tanzania kwa kupoteza Sh trilioni 1.5 kila mwaka kutokana na kufutwa kwa ushuru wa forodha na hakutakuwa na fidia yoyote ya upotevu huo wa fedha.

Alisema upotevu huo utatokana na kufutwa kwa ushuru wa forodha kulingana na masharti ya mkataba huo ambao utalazimu bidhaa zote kutoka jumuiya hiyo kuingia bure nchini.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi