loader
Picha

Hongera JPM kuhamishia Serikali Dodoma

HAYAWI hayawi yamekuwa. Rais John Magufuli ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuifanya Dodoma makao makuu mapya ya serikali yetu.

Miaka 46 tangu Mwalimu Nyerere atangaze nia ya serikali kuhamishia makao makuu yake huko, Rais Magufuli ndio katimiza ndoto juzi.

Akizindua mji wa Serikali eneo la Ihumwa, Kata ya Mitumba, kilomita 17 jijini Dodoma juzi, Rais Magufuli alisema amekuwa mtu mwenye furaha baada ya kuona anatimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere, jambo ambalo ni heshima.

Tunaungana na wananchi wengine kushangilia kujengwa kwa mji wa kiserikali kulikojengwa ofisi za wizara zote na pia uzinduzi wa jengo la ofisi ya Rais lililopo eneo la Ikulu, Chamwino.

Kujengwa na kuzinduliwa kwa majengo hayo kunazidi kuchagiza maendeleo ambayo serikali ya awamu ya tano imepania kuwapa wananchi.

Ndio maana tunasema, tunawiwa kumpongeza Rais Magufuli, wasaidizi wake, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri kwa kazi nzuri.

Pia tunawapongeza askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na la Kujenga Taifa (JKT) chini ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa kikosi cha JKT kilichojenga nyumba hizo, Brigedia Jenerali Charles Mbuge kwa kusimamia na kuimaliza haraka.

Askari hao wameonesha nchi ina hazina ya watendaji wazuri jeshini wenye uwezo mkubwa wa kusimamia miradi ya maendeleo vizuri.

Kazi yao imeharakisha ndoto ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhamira ya Rais Magufuli kukamilisha mradi huo kuenzi mchango wake hivyo kwao wote tunasema hongera na asanteni sana.

Kwa kuwa sasa Serikali ni rasmi Dodoma, ni wajibu wa kila mtu kujipanga kupata huduma zake huko kama lengo lilivyokuwa tangu awali.

Hatutarajii kuwepo kwa watu watakaoendelea kutoa visingizio vya kukosa ofisi Dodoma wakati Rais Magufuli amesema hata huduma za jamii kama hospitali, miradi ya maji, umeme, masoko, vituo vya mabasi, bandari kavu na uwanja wa mpira wa kimataifa vitakuwepo.

Ni wajibu wa kila mwananchi kujipanga sasa kunufaika na uwepo wa mji mpya wa serikali kwa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika biashara na sekta nyingine za maendeleo.

Kwa kufanya hivyo, wananchi watachagiza zaidi maendeleo ya kasi ya nchi ukizingatia kuwa Dar es Salaam ilionekana kuelemewa na hivyo sasa itapumua na kukua kwa nafasi zaidi.

Pongezi nyingine ziwaendee wabunge na Spika Job Ndugai kwa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuhakikisha ndoto hii inatimia.

Ni matarajio yetu Bunge litaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha nchi inapaa zaidi katika matamanio na matarajio yake ya maendeleo na ustawi wa jamii kupitia uchumi wa viwanda.

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi