loader
Picha

Serengeti yaanza vibaya Afcon

TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, jana ilianza vibaya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya kufungwa mabao 5-4 na Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na mabao mengi, timu zote zilicheza kandanda safi na kama vijana wa Serengeti wangezidisha umakini walikuwa na uwezo wa kutoka sare na wenzao ama kushinda.

Matokeo hayo yanaiweka Serengeti kwenye wakati mgumu kwani sasa italazimika kushinda mechi mbili zilizosalia dhidi ya Angola na Uganda ili ifuzu nusu fainali na kukata tiketi ya fainali za kombe la dunia.

Mabao ya Serengeti jana yaliwekwa kimyani na Edmund John akifunga mawili Kelvin John na Morice Ibraham wakifunga bao moja moja.

Kwa upande wa Nigeria mabao yao yalifungwa na Olatomi Olaniyan, Wisdom Ubani aliyefunga mabao mawili, huku Akinkunmi Amoo na Ibraheem Jabaar wakifunga bao moja moja.

Mechi hiyo ilianza kwa kasi na Nigeria wakianza kupoteza nafasi mbili za wazi ikiwemo ile ya dakika ya kwanza ambapo Wisdom Uban alishindwa kumalizia kufunga akiwa amebaki na kipa wa Serengeti Boys.

Nigeria walianza kuutawala mchezo huo kwa kufanya mashambulizi langoni mwa Tanzania katika dakika 20 za mwanzo na kupata bao la uongozi likifungwa Olaniyan lakini na Serengeti kusawazisha dakika moja baadae kupitia kwa John aliyeunganisha vizuri pasi ya Domonic William.

Nigeria waliendelea kulishambulia lango la Serengeti na Uban alirejea tena wavuni kwa kuifungia bao la pili dakika ya 29 baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Serengeti na kuuweka mpira wavuni.

Nigeria waliendelea kulisakama lango la Serengeti katika dakika ya 36 ambapo Amoo aliifungia bao la tatu baada ya kutumia vyema udhaifu wa walinzi kwa kumlamba chenga na kufunga kipa wa Serengeti Boys, Mwinyi Yahya.

John alifunga bao la pili kwa Serengeti Boys akipiga shuti kali lililomshinda kipa wa Nigeria, Seleman Shaibu.

Dakika ya 56 Morice Abraham aliisawazishia Serengeti bao la tatu kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi baada ya Edso Mshirakandi kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Mwamuzi alitoa penalti ya pili kwa Serengeti iliyofungwa na John dakika ya 59.

Wakati Serengeti wakidhani wamemaliza kazi, dakika ya 72 Nigeria walisawazisha bao hilo la nne baada ya Uban kuchonga mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja kwenye nyavu za Serengeti.

Kitendo cha kusawazisha bao hilo kiliwapa nguvu vijana wa Nigeria ambapo dakika ya 78 Jabaar aliifungia bao la tano kwa shuti kali.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi