loader
Picha

Aussems - Mazembe walitushinda uzoefu

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kutokuwa na uzoefu wa kutosha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni chanzo cha kupoteza mchezo wa marudiano wa robo fainali dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Mchezo huo wa marudiano ulipigwa mjini Lubumbashi ambapo Simba walipoteza mechi hiyo ya ugenini kwa kufungwa mabao 4-1 na kutolewa kwenye michuano hiyo baada ya kutoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Rekodi ya kupoteza michezo ya ugenini kwa mabao mengi imeonekana kuisumbua Simba kwenye michuano hii ambapo kwenye kampeni zake ilishinda mechi moja tu ugenini dhidi ya Mbabane Swallows ya eSwatini.

Aussems alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu kwao kwa kuwa wapinzani wao wana uzoefu hasa kwenye michezo ya hatua hiyo na kwamba wametolewa na wanajipanga wakiamini msimu ujao watakuwa na uzoefu baada ya kuona changamoto.

“Mchezo tulianza vizuri tulipata bao la mapema lakini wachezaji wangu walishindwa kulinda ushindi kutokana na wapinzani wetu kucheza kwa kumiliki mpira wakati wote hasa sehemu ya kiungo na kupata ushindi walioupata,” amesema Aussems.

Alisema kwa sasa nguvu zao wanaelekeza kwenye Ligi Kuu Bara kuhakikisha wanashinda mechi zilizobaki ili kutetea taji hilo na mwakani wapate tena tiketi ya kushiriki michuano hiyo.

“Saa hizi nguvu tunahamishia kwenye michezo ya ligi, tunajua tuna ratiba ngumu kwa kuwa tuna michezo 16 kutokana na ratiba yetu kuwa ngumu lakini tutajitahidi kila namna kupata ushindi utakaotuweka vizuri kwenye kutetea ubingwa wetu,” alisema.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi