loader
Picha

Samata- Senegal, Aljeria zitatupaisha

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samata amesema watapambana na Algeria na Senegal kwa lengo la kujiinua kisoka.

Samata ameyasema hayo siku chache baada ya droo ya fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ kupangwa na Tanzania kuwekwa kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya. Fainali hizo zitafanyika Misri kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19 mwaka huu.

Akizungumzia droo hiyo, Samata alisema Senegal na Algeria ni timu ngumu katika kundi lao lakini watapambana ili washinde waweze kuinua soka la nchi.

“Algeria na Senegal wamepiga hatua katika soka miaka mingi, hivyo ni lazima tuwaheshimu lakini ni lazima tupambane kuonesha tunakwenda walipo na tuna uchu wa kufika huko,” alisema Samata.

Pia Samata amesema wanaiheshimu Kenya kwa sababu ni majirani ila hawajaipita Tanzania.

“Tunawaheshimu Kenya ni majirani zetu wako vizuri katika maendeleo ya soka, lakini hawajafika mbali sana kuipita Tanzania,” amesema.

Aidha amesema Kundi C ni gumu, kwani linawakutanisha na timu kubwa za Afrika zilizowapita katika viwango kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kukawa na maandalizi madhubuti ili kushindana na kujaribu kupenya katika hatua ya mtoano na Tanzania inatakiwa kujiwekea malengo ya kushiriki kila fainali za AFCON kuanzia sasa.

Taifa Stars ilifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi nane, nyuma ya Uganda walioongoza kwa pointi 13 na kuiacha Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi