loader
Picha

Kinara mabao TPL atamani kucheza nje

MSHAMBUALIAJI wa Mwadui FC, Salum Aiyee amesema licha ya kuendelea kuwa kinara katika upachikaji wa mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara bado akili yake inawaza kwenda kucheza soka la kulipwa nje.

Aiyee hadi sasa amefunga mabao 16 yanayomfanya kuwa kinara katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akifukuziwa kwa ukaribu na Heritier Makambo wa Yanga kwa mabao 15 huku mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 14 akishika nafasi ya tatu.

Aiyee alisema bado ligi ni ngumu kwenye kila mechi anayocheza na amekiri wapinzani wake wanamkamia kwa kumchunga kwa makini asilete madhara, lakini bado anajitahidi kutumia vyema nafasi anayoipata kufunga na kuisaidia timu yake kupata pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo.

“Ni kweli mbio za ubingwa bado ngumu kwangu kutokana na kasi wanayokuja nayo washambuliaji kutoka Simba na Yanga na wana faida ya michezo mingi lakini ninachohitaji kwa sasa ni kufikisha mabao 20 ambayo naamini kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu ninakila sababu ya kufikisha,” alisema Aiyee.

Alisema anachokiangalia kwa sasa kutumia vema nafasi anazopata na hawaangalii wachezaji wanaomkaribia kwenye mbio hizo na kwamba anacheza ligi hiyo kwa malengo ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

“Siku zote kila mchezaji anahitaji mafanikio na huwa anacheza kwa malengo hata mimi nimejiwekea malengo ya kwenda kucheza nje ya nchi soka la kulipwa ili nifanikiwe kwenye maisha yangu na kutimiza ndoto niliyojiwekea,” alisema.

Mchango wa upachikaji wa mabao kwa mshambuliaji huyo umeisaidia timu yake kushika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20 baada ya kufikisha pointi 37sawa na Alliance, Mbao na Mbeya City.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi