loader
Picha

Wanafunzi wafundishwa kuomba mikopo

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza kuendesha programu za elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu sifa na taratibu za kuomba mikopo.

Akizungumza wilayani Maswa, mkoani Simiyu jana na wanafunzi 1,166 wa kidato cha sita kutoka shule zote 12 za mkoa huo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema uendeshaji wa programu hizo unalenga kuondokana na changamoto wanazopata wanafunzi wakati wa kuomba mikopo ya elimu ya juu.

HESLB ilianza kuendesha programu hizo katika mkoa wa Dar es Salaam. Wanafunzi hao wapo katika kambi iliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha sita inayotarajiwa kufanyika mwezi Mei. Kambi hiyo ipo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

"Uzoefu wetu na maoni ya wadau wetu umetufanya tuanzishe programu hizi nchini kote ili wakati wa kuomba mikopo, muombe kwa usahihi na wale wenye sifa wapate na hatimaye kutimiza ndoto zao," aliwaambia wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa Badru, katika mwaka wa masomo 2018/19, kati ya waombaji wa mikopo zaidi ya 57,000 ambao walipata udahili vyuoni, maombi zaidi ya 9,000 yalikuwa na upungufu mkubwa, ikiwemo kukosa nyaraka kama vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho sahihi vya wadhamini, kutosainiwa na waombaji, wadhamini au serikali za mitaa au vijiji.

Akizungumza na wanafunzi hao, Ofisa Mikopo Mwandamizi kutoka HESLB, Daudi Elisha aliwasihi wanafunzi hao kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na HESLB mwezi ujao ambao utaeleza hatua kwa hatua kuhusu uombaji wa mkopo.

Akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dk Seif Shekalaghe aliishukuru HESLB kwa kutambua changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na kuamua kuzitatua.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watan-

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Maswa

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi