loader
Picha

Zantel yapata vyeti ubora wa kimataifa

KAMPUNI ya mawasiliano ya Zantel imepata vyeti viwili vya ubora wa kimataifa (ISO) kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa katika kuendesha kwa ufasaha biashara zake.

Cheti cha kwanza ni cha kuzingatia utunzaji wa mazingira (ISO 14001:25) na kingine ni cheti kipya cha utekelezaji wa mifumo ya afya na usalama mahali pa kazi (ISO 45001:2018).

Mafanikio hayo ni mwendelezo, ambapo mwaka jana mwishoni baada ya kufanyiwa ukaguzi, ilipata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kukidhi vigezo vya utekelezaji mifumo ya afya na usalama mahali pa kazi kwa ufasaha (OHSA 18001:2007).

Kutokana na ukaguzi huo, ilibainika inatekeleza vizuri mifumo ya afya na usalama.

Wakaguzi walipendekeza Zantel ibadilike kutoka cheti cha zamani cha OHSA 18001:2007 na kupatiwa cheti kipya cha ISO, ambacho kimeanza kutolewa kwa makampuni yanayokidhi vigezo mwaka jana.

Akizungumzia mafanikio hayo ya kampuni kupata vyeti vya kimataifa vya ISO, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia Mawasiliano wa Zantel, John Sicilima alisema wanayo furaha kuweza kukidhi viwango vya ukaguzi na kupata vyeti hivyo vya ubora wa kimataifa.

“Hatua hii inadhihirisha umakini wetu wa jinsi tunavyozingatia suala la afya na usalama kuanzia kwa wafanyakazi, wadau mbalimbali tunaoshirikiana nao katika mazingira tunayofanyia shughuli zetu,” alisema.

Alisema moja ya malengo waliyojiwekea ni kuendesha shughuli zao huku wakilinda usalama wa jamii katika maeneo wanayofanyia biashara sambamba na kuongeza hadhi ya kampuni hiyo.

Alisema baada ya kupata vyeti vya kimataifa vya ISO, Zantel itahakikisha inafanikisha dhamira yake katika maeneo ya afya na tahadhari katika usalama, athari za mazingira, kutekeleza kanuni za usalama kwa vitendo, mifumo ya uharibifu wa mazingira wa sauti na kuhakikisha tahadhari zaidi na athari zinadhibitiwa ipasavyo.

“Utekelezaji wa maelekezo yanayoendana na vyeti hivi yatawezesha taswira ya Zantel kuwa nzuri zaidi, kuongeza uhusiano mzuri na jamii na kupanua wigo wa masoko ya biashara zetu na wadau wengine,” aliongeza Sicilima.

Taasisi yenye cheti cha kimataifa cha ubora cha ISO 45001, inapaswa kuwa inatekeleza mifumo ya afya na usalama kwa ufasaha, lengo kuu likiwa ni kulinda afya na usalama kwa wafanyakazi na watu wengine.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema yeyote atakayewekeza mkoani Pwani hatajuta.

Amesema ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi