loader
Picha

IGP: Polisi msinyanyase raia

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewataka askari wa jeshi hilo kuacha kupokea rushwa na kutonyanyasa raia.

IGP amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na viongozi wa jeshi hilo Mkoa wa Morogoro.

Amesema hayo kwenye ziara ya ghafla ya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari zilizojengwa kutokana na michango, iliyowashirikisha wadau wa maendeleo.

Amesema watu wakifanya kazi bila woga, kutokana na kuwepo kwa usalama wao na mali zao, wanakuwa mstari wa mbele kuliunga mkono jeshi lao, kama wadau wengi hivi sasa wanavyotoa michango yao ili kujenga na kukarabati nyumba za askari wa Morogoro.

Kwa upande wa ulinzi na usalama wa raia kwa Morogoro, amesema Mkoa wa Morogoro ni shwari, ila wananchi wasibweteke, kwa sababu hata matukio yaliyotokea Kibiti mkoani Pwani, historia yake inaonesha yalianzia kwenye mapori ya Morogoro.

“Watu wachache wanaotaka kutuletea shida bado wapo, ni vyema kila mmoja wetu kumjua jirani yake na pale unapomtilia shaka ni vyema kutoa ripoti kwa vyombo vya ulinzi na usalama hasa Polisi," amesema IGP Sirro.

Aliwakumbusha wenye nyumba pale wanapopangisha wateja wao, wawe na mikataba yenye picha zao ili kuepuka usumbufu baadaye.

Alisema wapo baadhi yao, wanaweza kutumia mwanya huo kufanya uhalifu, kama ambao unaonekana sasa katika nchi jirani na baadaye wakatoweka bila ya kufahamika.

"Ni vyema wananchi tukawa makini kwenye mitaa kuwatambua watu wenye nia ovu, na Kamati za Ulinzi za Mitaa, Vijiji, Kata na Tarafa zifanye kazi zao na wakiona kuna jambo si la kawaida ni vyema kupeana taarifa.

Katika hatua nyingine, Sirro amesema ofisi yake imetoa Sh milioni 10 zitakazosaidia katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba 10 za askari wa jeshi hilo mkoani Morogoro.

Amesema lengo ni kuwezesha nyumba hizo ziweze kuanza kutumika ifikapo Mei 31, mwaka huu.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi