loader
Picha

Gavana: Elimu ya fedha muhimu kwa wakopaji

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amesema elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo wa taarifa za mikopo ili kuwawezesha Watanzania kupanga matumizi bora ya mikopo.

Profesa Luoga alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma kuhusu taarifa za mikopo na fedha, iliyoratibiwa na BoT kwa kushirikiana na International Finance Corporation (IFC), ambayo ni moja ya taasisi za Benki ya Dunia.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Philip Mpango, Prof Luoga alisema taarifa za mikopo na elimu ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha Watanzania wanaondokana na matumizi ya anasa ya mikopo.

“Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini,” alisema.

Meneja Msaidizi wa Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina alisema kampeni hiyo ya miezi mitatu, inalenga kuongeza uelewa, mwamko kuhusu taarifa za mikopo na kukuza upatikanaji wa mikopo.

”Kaulimbiu katika kampeni hiyo ni: “Pata Taarifa Yako ya Mikopo Leo. Angalia hali yako ya kifedha ili kupanga mustakabali wako bora wa kesho” inaungwa mkono na wadau mbalimbali katika sekta ya huduma za fedha.

“Wadau hao wameahidi kusaidia kusambaza ujumbe kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa mikopo na jinsi Watanzania wanavyoweza kuishi maisha bora kwa kuweza kupata taarifa za mikopo yao na kujua historia ya mikopo yao,” amesema.

Alisema usimamizi mzuri wa mikopo na historia nzuri ya mikopo ni muhimu katika kuwezesha kupata mkopo nafuu.

"Kuhakiki taarifa yako ya mikopo mara moja kwa mwaka ni huduma inayopatikana bila malipo, tena itakuletea mafanikio kwa kukuandaa vema utakapoenda kuomba mkopo.

"Historia nzuri ya mikopo inaweza kusaidia kustahili viwango vya chini vya riba na ada, hivyo kuondokana na kutenga fedha kwa ajili ya dharura na gharama zisizotarajiwa," amesema.

Alisema mikopo inasaidia kupata mahitaji ya sasa, kama vile nyumba au ada ya shule kwa watoto, kwa kuzingatia ahadi ya kulipa kwa awamu na kwa muda uliopangwa.

Meneja wa IFC Tanzania, Manuel Moses amesema taarifa ya mikopo inaonesha taarifa binafsi, utambulisho na taarifa ya mawasiliano na ikiwezekana historia ya ajira, idadi na aina za akaunti za mikopo.

Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Dun & Bradstreet, Josephine Temu alisema kwa sasa kuna taasisi mbili zilizopatiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania kuandaa na kutoa taarifa za mikopo Tanzania, ambazo ni Creditinfo Tanzania Limited na Dun & Bradstreet.

Alisema taasisi hizo zinakusanya na kutunza taarifa za mikopo na kutoa taarifa za mikopo kwa kampuni au watu wanaozihitaji kama vile benki.

Alisema ripoti hiyo ya mikopo, inaweza kutolewa na taasisi hizo mara moja kwa mwaka bila malipo.

Akifafanua kuhusu mambo muhimu ya kuangalia kwenye taarifa ya mikopo, Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Creditinfo, Tonny Missokia amesema muhimu ni taarifa binafsi kama vile jina, ndoa, anwani, taarifa za ajira na namba za mawasiliano ni sahihi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema yeyote atakayewekeza mkoani Pwani hatajuta.

Amesema ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi