loader
Picha

TRA yakusanya tril 4 miezi mitatu

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kati ya Januari hadi Machi mwaka huu imekusanya shilingi trilioni 3.96/-.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Richard Kayombo ameyasema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari mchana jijini Dar es Salaam.

Kayombo amesema, TRA imefanikiwa kukuanya jumla ya trilioni 11.96 katika kipindi cha miezi tisa ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai 2018 hadi Machi mwaka huu.

“TRA inawashukuru walipakodi wote kwa kulipa kodi zao kwa hiyari na kwa wakati, tunahimiza wote ambao wanasuasua kujitokeza na kulipa kodi hizo,” amesema.

Kayombo pia ametoa wito kwa ambao hawajalipa kodi za majengo, kufanya hivyo ili waepuke usumbufu wa kulipa mwishoni kwa kuwa sasa viwango ni rafiki na vinalipika.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi