loader
Picha

Shahidi adai mbio alizotimua Mbowe hajawahi kuona tangu azaliwe

MRAKIBU Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliamuru askari kupiga mabomu ya moshi na risasi za moto hewani kwa ajili ya kusambaratisha maandamano ya viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alidai katika maandamano hayo yaliyofanyika Februari 16, mwaka jana wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni, baada ya kupigwa kwa risasi hewani, hakuamini kama Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa na mbio kiasi kile, kwa sababu mbio alizotimua, hajawahi kuona tangu azaliwe. Ngiichi ambaye ni Ofisa Operesheni wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi, inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, Ngiichi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa tarehe hiyo ilikuwa ni siku ya kufunga kampeni za uchaguzi, ambapo kulikuwa na mikutano mikubwa mitatu ya Chama cha Wananchi (CUF) iliyofanyika viwanja vya Vegas Makumbusho, mkutano wa Chadema ulikuwa viwanja vya Buibui Mwananyamala na mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ulifanyika viwanja vya Biafra Kinondoni.

Alidai pamoja na kuimarisha ulinzi katika mikutano hiyo ya kampeni, viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, waliwaongoza wafuasi wao kuandamana kutoka kwenye viwanja vya kampeni kwenda ofisi za Mkurugenzi wa Kinondoni, ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi.

“Katika mikutano hii nilipanga maofisa wa kusimamia kampeni hizi ambapo mkutano wa Chadema ulisimamiwa na SSP Dotto, mkutano wa CUF ulisimamiwa na SP Batseba na wa CCM ulisimamiwa na SP Magai. “Lakini kati ya saa 11:30 kwenda saa 12 jioni nilipewa taarifa na Dotto kuwa kwenye mkutano wa Chadema kuna dalili za kuwepo kwa uvunjifu wa amani kwa sababu viongozi wanaopanda majukwaani wanahamasisha chuki na uvunjifu wa amani,” alidai Ngiichi.

Alidai kuwa alimuelekeza ofisa huyo, kusimamia kwa weledi mkutano huo na kuelekeza askari kuchukua kumbukumbu ya vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa. Ofisa huyo alidai baada ya kutoa maelekezo hayo, alipigiwa simu na kuelezwa kuwa viongozi wa Chadema, walikuwa wakihamasisha wananchi kuondoka kwenye mkutano na kwenda kwa Mkurugenzi wa Kinondoni.

“Kwa mara nyingine nilimwambia SSP Dotto awaonye viongozi hao kwamba kinachoendelea ni mkutano na si kuondoka kwenda kwenye eneo lingine kwa sababu hawajajipanga na muda huo ofisi za serikali zilikuwa zimefungwa, lakini walikataa na kuhamasishana kuondoka kwenda barabarani,” alidai. Kutokana na hali hiyo, Ngiichi alidai kwamba aliita askari wengine, ikiwemo kutoka vikosi vya doria, magari, pikipiki na wa usalama barabarani kwenda kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Mwananyamala, kuzuia maandamano hayo na kwamba Mbowe na wenzake walikaidi amri iliyotolewa.

SERIKALI imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi